Mashindano ya Insha Zanzibar kupewa kipaumbele kwa Wanafunzi wa Sekondari
WANAFUNZI Wa Skuli Za Sekondari
Zanzibar wametakiwa kufikiria masomo yao zaidi na
kuacha vitendo ambavyo vitapelekea kupunguza juhudi za kushughulikia
masomo hatua ambayo itapunguza ufaulu katika mitihani yao .
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mjini
Magharibi katika Mashindano ya utungaji wa Insha kwa
Wanafunzi wa Kidato cha Tatu na Nne
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A
Captein Khatib Khamis Amesema Wanafunzi wengi
wamekuwa wakizarau Masomo yao na kushughulikia
Michezo ambayo haina manufaaa ndani ya
maisha.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya
Amelitaka Shirika La Bima Zanzibar Kupeleka
Ushawishi Kwa Mashirika Mengine katika kuunga
mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza Elimu hususani
katika mitihani ya majaribio
kwa lengo la kupata wataalamu
waliobobea katika fani mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya
Michezo na Utamaduni Zanzibar Hassan Tawakal
Hairallah amesema kuwa Wizara ya Elimu kupitia idara ya
Michezo Zanzibar itahakikisha inaunga mkono
mashindano ya insha yanayotolewa kila mwaka
ili kukuza Michezo katika Skuli Zote
Za Visiwa Vya Zanzibar .
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Bima Zanzibar Abdulnasir
Abdulrahmani amesema kuwa Shirika hilo litaendelea
kushirikiana na Wizara ya Elimu katika
shughuli mbalimbali ili kuona sekta hiyo inaendelea kukuza vipaji vya wanafunzi
katika nyanja tofauti.
Wakizungumza mara baada ufunguzi wa shindano hilo
baadhi ya Wanafunzi wa Skuli za
Sekondari wameishukuru Wizara ya Elimu kwa kuwawekea
Mashindano hayo ambayo yanaweza kukuza
akili na kusababisha ufaulu kwa
wanafunzi wengi .
Katika Mashindano hayo yatajumuisha
zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Pesa
Shilingi laki Tatu kwa Mshindi w
Mwanzo , Laptop, Mabuku Arobaini na Mkoba wa
Skuli.
Post a Comment