'Tatizo la Upatikanaji wa Maji kwa Wananchi Micheweni limeisha'
TATIZO
la uhaba wa Maji linalowakabili wananchi wa Shehia za Majenzi Wilaya ya
Micheweni limeanza kutafutiwa ufumbuzi baada ya zoezi la uwekaji wa Mifereji ya
Maji na Matanki katika Maeneo hayo kuanza.
Bi
Nyota Kombo Rashid, Mmoja wa Wananchi hao akizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI amesema
kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawapunguzia matatizo wanayokumbana nayo akinamama
wa shehia hizo kutokana na uhaba wa Maji.
Sheha
wa Shehia hiyo ya Majenzi, Fakh Kombo Hamad, amesema kupatikana kwa mradi huo ni
hatua kubwa kwa wananchi wa shehia hiyo kwani wamekuwa wakikabiliwa na Matatizo
mbalimbali kwa Mda mrefu.
Akizungumza
wakati wa zoezi la uwekaji wa mifrereji hiyo, Afisa wa Maji Wilaya ya
Micheweni, Ali Rajab Khalid, amewataka wananchi kuitunza na kuilinda
miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Awali
akizungumza na Wananchi, Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni ambae Pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
maaalumu za SMZ Mh. Shamata Shaame Khamis, amesema hatua hiyo ni moja ya juhudi zinazoendelea kufanywa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutatua kero za Wananchi wake.
![]() |
Baadhi ya wanachi walioshiriki zoezi hilo wakiendelea na uchimbaji ma mfereji huo. (PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES- MICHEWENI RADIO)
|
Post a Comment