Header Ads

Vijana Micheweni: Tunaishukuru ActionAid kutupatia Elimu hii


VIJANA katika Wilaya ya Micheweni wamelipongeza Shirika la ActionAid kwa kuendelea kuwapatia Elimu juu ya Masuala ya Kidemokrasia, Utawala Bora na Haki za Binaadam kwani elimu hiyo inawasaidia kufahamu mabo mbalimbali.

Wakizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI mara baada ya kumalizika kwa Mdahalo wa Mafunzo uliowakutanisha vijana hao katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Micheweni wamesema kuwa Elimu hiyo imewawezesha kujifunza mambo muhimu juu ya Demokrasia na Utawala Bora.

Kwa upande wake Mariam Ahmad Omar amesema mafunzo hayo ameya[pokea vizuri na yamebadilisha mtazamo aliokuwa nao kabla ya kupatiwa elimu hiyo.

Mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kwa wananchi wa wilaya ya Micheweni juu ya Mradi wa Action Aid ambayo yanaendeshwa na Wafanyakazi wa Shirika hilo.

No comments