Uharibifu katika Msitu wa Ngezi Wilaya ya Micheweni Ulivyoanza kuathiri Vijiji 12, Wananchi wataja Sababu zake
WAKAAZI wa Vijiji
12 vinavyozunguka Msitu wa hifadhi ya Serikali wa Ngezi katika Wilaya ya Micheweni
wamesema vitendo vya baadhi ya wananchi kutumia fursa ya uwepo na msitu
huo kuharibu mazingira kumeanza kupunguza neema zinazopatikana na ndani
ya hifadhi hiyo .
Baadhi ya
wananchi wamekuwa wakitumia msitu huo kama maficho ya kufanyia uhalifu wa
kutengeneza pombe haramu aina ya Gongo, na kusababisha kutoweka kwa baadhi miti
ya matunda na viumbe hai.
Hali hiyo
inaweza kusababisha umaskini kwa baadhi ya wananchi ambao wanategemea uwepo na
viumbe hai pamoja na miti ya matunda matunda hayo kuendesha maisha yao.
Neema ambazo
tayari zimeanza kutoweka ni pamoja na viumbe hai wanaopatikana kwenye maziwa
yaliyomo ndani ya hifadhi wakiwemo Kambare pamoja na miti ya matunda aina
ya Mabungo.
Wakizungumza
na REDIO JAMII MICHEWENI wametaja athari nyengine kuwa ni kupungua matunda
aina ya mabungo ambayo ni maarufu kwa kinywaji kinachopendwa na wengi cha juisi
.
Hamad
Bakar, amesema kuwa Mabungo ambayo awali yalikuwa yanapatikana
kwa wingi ndani ya hifadhi hiyo kwa sasa yameanza kuwa adimu kupatikana.
“Ukifika
msimu wa mabungo vijana wengi hujiimarisha kiuchumi na maisha yao kuwa bora
kutokana na matunda hayo kuchumwa kwa wingi na kuinufaisha jamii yote kisiwani
Pemba lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti” alieleza.
Akizungumzia
hali hiyo Afisa Mkuu wa Msitu huo Abdi Mzee amekiri kuwepo na baadhi ya
wananchi wanautumia msitu kama maficho yaona kueleza kuanza kutoweka kwa
viumbe hai wakiwemo vyura na samaki aina ya kambare.
Abdi amesema
kuwa licha ya vitendo hivyo kupungua siku hadi lakini tayari athari hizo
zimeanza kujitokeza jambo ambalo pia limekuwa likiathiri sekta ya Utalii kwani
watalii wengi wanaotembelea msitu hupenda kuangalia viumbe hai ndani ya maziwa
pamoja na matunda aina ya mabungo.
“Viumbe hai
wegi wanaopatikana kwenye maziwa ndani ya hifadhi , kutokana na wapikaji wa
gongo kumwaga maji machafu yanayotokana na vitendo vya upikaji wa pombe haramu’’alifahamisha
.
Aidha
ameeleza kwamba mbali na kuanza kutowekwa kwa viumbe hao , piamajanga ya
kuungua moto msitu huo yamekuwa yakitokea na kuchangia athari kimazingira .
Kupungua kwa
matendo ya uharibifu ndani ya hifadhi hiyo , kimetokana na operesheni
inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib ya kuwasaka na
kuwakamata wananchi wanaoendesha vitendo hivyo kwenye hifadhi ya msitu wa Ngezi
.
Post a Comment