ZAECA: 'Kupiga Vita dhidi ya Rushwa, Uhujumu wa Uchumi Zanzibar ni Jukumu la kila Mmoja'
BAADHI ya Vijana katika Wilaya ya
Micheweni wamesema bado itachukua muda kuweza kufanikisha vita dhidi ya rushwa
kwa kuwa wapo wananchi wanaochangia kutoa rushwa bila ya kudaiwa.
Wakizungumza na Redio
Jamii Micheweni wamesema ili mapambano dhidi ya vitendo
vya rushwa na uhujumu wa uchumi yaweze kufanikiwa ni budi jamii
kuhakikisha inashiriki kupiga vita matendo hayo.
Khatib Omar Khatib –KITATANGE– amesema
wakati mwengine jamii inachangiaa kuwepo na matendo hayo .
Aidha Hamad Ali Hamad ameitaka jamii
kila mmoja kwa mujibu wa nafasi aliyonayo kushiriki kupiga vita dhidi ya rushwa
na uhujumu wa Uchumi kwani huu sio wakati wa kutoa kitu kwa lengo la kupata
kitu .
Naye Mariam Salim Juma amesema vitendo
vya rushwa na uhujumu wa uchumi husababisha mwenye haki kukosa haki.
Mdhamini wa mamlaka ya kuzuia rushwa na
uhujumu wa uchumi Zanzibar, -ZAECA- Mkoa wa Kaskazini Pemba Abubakar Mohamed
Lunda amesema bado mamlaka hiyo inakosa taarifa sahihi na kuwataka wananchi
kushirikiana na mamlaka hiyo kuyatokomeza matendo hayo .
Post a Comment