Mjimkongwe kufanyiwa Marekebisho
MKURUGENZI wa
Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, Issa Sarboko Makarani
amesema wanatarajia kulifanyia matengenezo makubwa nyumba ya Bait al Ajab ili
kurejesha hadhi kama ilivyokua hapo kabla.
Akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kumalizika ziara ya ujumbe kutoka serikali ya Oman
uliotembelea nyumba mbali za kihistoaria zilizopo katika mji Mkongwe.
Alisema lengo la
ujumbe huo kujua hali ya ubovu na mpangilio mzima unaotaka kufanywa katika
majumba hayo katika uendelezaji wa mashirikiano yao na Serikali ya Zanzibar
katika kuimarisha Utamaduni.
Alisema majengo
hayo yatakapokamilika kufanyiwa matengenezo na wataalamu yatasaidia kuweka mji
katika hali ya ubora na kupatikana kuongezeka kwa watalii.
Pia alisema
ushirikiano wa wajumbe hao utaleta mafanikio katika kutembelea sehemu za
kihistoria kwani utaleta mchango mkubwa katika kuimarisha Utalii.
Alisema timu ya
wataalamu ipo kamilifu kushirikiana na wataalamu wazoefu ili kuhakikisha katika
ziara yao hiyo ya siku tano kuweka utaratibu wa matengenezo unaohitajika
ili kuongezeka kwa watalii katika kisiwa cha Unguja.
Post a Comment