Meli ya pili inayobeba ndege ya China yafanyiwa majaribio baharini
MELI ya pili inayobeba ndege
za kivita ya China leo imefunga safari kutoka bandari ya viwanda vya
utengekezaji wa meli ya Dalian na kufanyiwa majaribio ya mfumo wa injini na
vifaa vyingine.
Habari zinasema kuwa, kazi ya
utengenezaji wa meli hiyo imeendelea kufuatia mpango uliopangwa baada ya terehe
26 Aprili mwaka jana ilipozinduliwa, na kukamilisha shughuli ya kubaini kasoro,
kufanya marekebisho ya mfumo na vifaa, utengenezaji na majaribio husika ya
nanga, na hatimaye sasa imekuwa na hali ya kiufundi ya kwenda baharini
kufanyiwa majaribio.
Post a Comment