'Tutaendelea kushirikiana na Serikali kuu Kutatua tatizo la Madawati'
MKUU wa mkoa wa mjini wa magharib mhe, Ayoub Mohammed Mahmuud amesema wataendelea kushirikiana na serikali kuu katika
kutatua tatizo la madawati kwa skuli za mkoa wa mjini ili kuimarisha ubora wa
elimu nchini
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara
maalumu katika eneo lililotengwa kwa ukati wa miti itakayotumika
kutengenezea madawati ya skuli za mkoa wa mjini alisema hatua hiyo
imekuja kutokana na upungufu wa madawati katika skuli za mkoa wa mjini
lilosababishwa na kuongezeka kwa madarasa mapya.
Alisema pamoja na serikali kuu kuhamasisha wadau
mbali mbali kuchangia upatikanaji wa madawati hayo, bado mkoa wa mjini
magharibi unahitaji wastani wa madawati 33,000 hivyo ili kukabiliana na
tatizo hilo ofisi yake imeamua kununua miti katika eneo la kichwele na
kuchana mbao ambazo zitatumika kutengenezea madawati hayo.
Aidha Mhe; Ayoub alisema hadi sasa mbao
elfu 2 zimeshapatikana ambapo kati ya hizo mbao 1,150 zimeshapakwa dawa
kwa ajili ya kutengezea madawati na kuwashukuru wadau mbali mbali walioitikia
wito wa kusaidia mchakato huo.
Kwa upande mwingine mhe, Ayoub ametoa wito
kwa wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya mkoa huo kuendelea kutoa michango yao
katika suala la elimu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kwa lengo na kukuza
kiwango cha elimu nchini.
Hata hivyo alisema kupitia njia hiyo mkoa
huo utaokoa zaidi ya shilingi 212,000 kwa dawati moja ambapo ekari 137
zinatarajiwa kuvunwa miti hiyo katika shamba la mipira la Kichwele kwa kutumia
mafundi kutoka idara maalum za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Nae Katibu Mtendaji wa kamati ya ukataji miti ya
mipira kwa ajili ya madawati Mkoa wa mjini Magharibi ndugu Mohammed Sheha
Kheir amesema katika zoezi hilo miti 3045 inatarajiwa kukatwa kwa ajili ya
kutengenezea madawati zaidi ya elfu 12.
Pia Katibu mtendaji huyo ameiomba serikali ya
mkoa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo viatu kwa ajili ya mvua na kuharakishwa
kupatiwa posho zao kwa ajili ya kujikimu kimaisha ili kufanya kazi
kwa ufanisi zaidi.
Ziara hiyo mkuu wa mkoa huyo ilimalizia katika
kiwanda cha SANA kinachotumika kutia dawa mbao kabla ya kuuanganishwa na
kuwa dawati lengo la kukabiliana na tatizo la madawati katika mkoa wake na
maeneo mengine kwa ujumla.
Post a Comment