DC WETE aagiza Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano kutatua kero ya miundombinu ya barabara wilayani humo
MKUU wa
Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali ameitaka Wizara ya Ujenzi Mawasiliano
na Usafirishaji Pemba kuchukua juhudi za makusudi ili kuhakikisha
wanaweka barabara mbadala ambayo itawasidia wananchi baada ya barabara
waliyokuwa wakitumika kuharibika.
Kauli
hiyo ameitoa wakati wakukagua barabara hiyo ya Gando ilivyoharibika
huko katika eneo la Mangwena shehia ya Bopwe akifuatana na kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya.
Amesema
barabara hiyo kwa hivi sasa imekuwa ni hatari kutumika hivyo ni
vyema kuchukua juhudi za haraka ili kutayarisha barabara ambayo itatumiwa na
wananchi katika kipindi hiki na kuendeleza shughuli zao za kawaida.
Aidha
ameliagiza jeshi la polisi katika wilaya hiyo kuweka doria katika barabara hiyo
ili kuwazuia wananchi ambao watapita katika eneo hilo.
Nae
Afisa msimamizi wa Barabara Wilaya ya Wete Masoud Ali Mussa ameahidi
kuchukua hatua za kuiboresha barabara ya zamani ili wananchi waweze kuitumia
katika kipindi hiki na huku wizara inachukua juhudi za maksudi juu ya barabara
hiyo.
Wananchi
wanaotumia barabara hiyo ya Gando wanaiomba Wizara ya Ujenzi
Mawasiliano na Usafirishaji Pemba kufanya utafiti wa kina
wakati wa kuirekebisha barabara hiyo ili kuepuka changamoto zinazopelekea
uharibifu wa barabara hiyo kila ifikapo kipindi cha mvua .
Post a Comment