RC KAS PEMBA: Askari wa Vyuo vya Mafunzo ongezeni juhudi kwenye kilimo
MKUU wa Mkoa
wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewataka Askari wa Vyuo Vya Mafunzo
Pemba kuongeza juhudi katika kuendeleza shughuli za kilimo
kwa kuunga mkono mikakati ya Serikali kuimarisha uzalishaji na
kupunguza uwagizaji wa chakula kutoka nje.
Akizindua
zoezi la uvunaji wa mpunga katika mabonde ya Tungamaa , Mhe Omar amewataka
askari wa vyuo vya Mafunzo kuweka mikakati ya kuzalisha kwa ushindani na vikosi
vyengine ili kuamsha ari ya kuzalisha chakula ambacho kitatosheleza
mahitaji ya wananchi.
Mkuu wa
mabonde vyuo vya Mafunzo Staff Sagenti Khamis Seif akitoa taarifa amesema
kuwa wataendeleza uzalishaji kupitia shughuli za kilimo ili kuona wanafikia
malengo yaliyowekwa na Serikali.
Uzinduzi
huo pia umehudhuriwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna
msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir Ali ambaye amepongeza juhudi zinazochukuliwa
na askari wa vyuo vya mafunzo.
Jumla
ya Tani kumi za mbunga zinatarajia kuvunwa na Kikosi cha Mafunzo katika Bonde
la Tungamaa Mkoa wa Kaskazini Pemba
Post a Comment