Uwajibikaji wahimizwa kuulinda Msitu wa Ngezi
UWAJIBIKAJI katika utoaji na upokeaji wa
huduma ndio njia pekee inayotoa muelekeo kwa Serikali kuweza kuwapatia
wananchi maendeleo yanayostahiki kwa wakati.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi ya
Msitu wa Ngezi Hassan Suleiman Khamis wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Serikali
kwenye ukumbi wa wizara ya elimu mkoa wa kaskazini pemba .
Amesema huduma zinaweza kuwa rahisi na kutolewa kwa
wakati iwapo kila mmoja atawajibna kuepuka malalamiko ya wananchi .
Mapema akitoa mada katika mafunzo hayo, katibu
wa jumuiya hiyo, Muhammed Nassor Salim, amesema kuwa jumuiya hio ina lengo la
kuwapa fursa wanajamii wakaweza kupaza sauti zao pamoja na kuelewa mikakati
inayochukuliwa na serikani katika kutatua matatizo yao.
Akichangia katika mafunzo hayo, kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Wete, Salma Abdul Hamad, amesema kuwa, bado
kunahitajika jitihada za makusudi zitakazoweza kuwabadilisha wanajamii na dhana
ya uwajibikaji katika utoaji wa huduma.
Mafunzo hayo ya siku moja, yaliandaliwa na jumuiya
ya uhifadhi wa maliasili ngezi pemba (NGENARECO) imewashirikisha viongozi wa
ngazi mbali mbali za serikali mkoa wa kaskazini pemba.
Post a Comment