Asakwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka Mtoto wa Miaka mitatu Pemba
JESHI
la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamsaka kwa udi na uvumba mtuhumiwa
anaedaiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na kumsababishia
maumivu sehemu zake za siri .
Tukio
hilo limetokea jini 24 mwaka huu , huko Shehia ya Bopwe Wilaya ya
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na mtuhumiwa kukimbia baada ya kutekeleza kitendo
hicho cha kinyama
Akizungumza
ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa Kaskazini Pemba Kamishna Msaidizi
mwandamizi Hassan Nassir Ali amesema jeshi la Polisi linafanya kila njia
ili kuhakikisha mtuhumiwa anapatikana na kufikishwa mahakamani .
Amesema
kwamba tayari askari wa kitengo cha upelelezi wameanza kufanya uchunguzi
wa kisayansi kumtafuta mtuhumiwa huyo na kuwataka wananchi kuwapa ushirikiano
utakaofanikisha kukamatwa tuhumiwa huyo.
‘’Tumejipanga
na tumeanza kufanya uchunguzi , cha msingi nawaomba sana wananchi washir8kiane
na askari kwa kutoa taarifa ambazo zitafanikisha mtuhumiwa huyo kutiwa
mikononi’’ alieleza .
Aidha
Kamanda Nassir amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufuatilia mienendo ya
watoto wao , jambo ambalo litasaidia udhibiti ongezeko la matendo ya ubakaji
ambayo huwaathiri zaidi kiafya.
Kamanda
Nassir amesema matendo ya udhalilishaji wa wanawake na watoto yanaweza kupatiwa
fumbuzi na kukomeshwa iwapo kila mmoja atawajibika kulingana na nafasi
aliyonayo.
Afisa
Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete , Haroub Suleiman Hemed ameishauri jamii
kshirikiana katika kuyapiga vita matendo ya udhalilshaji yakiwemo ya ubakaji wa
wanawake na watoto .
Haroub
amesema pamoja na elimu inayotolewa na taasisi za umma na binafsi lakini bado
wapo baadhi ya wananchi wameshindwa kuipokea taaluma hiyo kwa mtizamo
unaokubalika na hivyo kuwa ni kikwazo katika mapambano dhidi ya matendo
hayo.
‘’Hili
si jukumu la mtu mmoja au serikali pekee , bali ni la kima mmoja ,
hivyo ushirikiano wa wanajamii wote unahitajika ili kufanikisha kufikia lengo
‘’ alifahamisha.
Haroub
amewaasa wanajamii kujiepusha na vitendo vya rushwa muhali bali wawe tayari
kushiriki kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria wanapohitajika , ili kuunga
mkono juhudi za serikali za kuyatokomza matendo hayo.
Hivyo
amepongeza uwamuzi wa Serikali wa kufuta dhamana kwa watuhumiwa na matendo ya
ubakaji wa wanawake na watoto na kusema kwamba hatua hiyo itasaidia katika
mapambano dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.
Post a Comment