ZECO Pemba yawataka Masheha Micheweni kuwaelimisha wananchi wao kuilinda miundombinu ya Umeme
SHIRIKA la
umeme kisiwani Pemba limewataka masheha
kuwaelimisha wananchi wao juu ya matumizi na sheria ya uungaji wa huduma hiyo
ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.
Akizungumza na
masheha huko ukumbi wa ZANGOC Wilaya ya
Micheweni Afisa uhusiano wa Shirika hilo Kisiwani Pemba Amour Salim
Massoud amesema kuna baadhi ya wananchi wanaitumia huduma hiyo kinyume na
malengo na kusahau umuhimu katika maendeleo.
Amour amesema umeme
si anasa bali ni huduma muhimu katika kuendesha sekta mbalimbali za kijamii
hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuitumia huduma hiyo kwa uangalifu na kulinda
miundo mbinu yake.
Mapema Afisa huduma
wa ZECO Pemba Amour Khalid amewasihi masheha kuzidi kuwaelimisha wananchi wao kwa kutowapa
fedha watu wasioeleweka katika kuungiwa umeme jambo ambalo limekuwa likileta
malalamiko kwa wateja kuwa shirika linawaibia.
Nao baadhi ya
Masheha hao wamesema pamoja na kutowa elimu kwa wananchi wao lakini nao
watendaji wa shirika la umeme wabadilike katika kutoa huduma kwani baadhi
hudharau miito wanapopewa taarifa na wateja ya kuungua au kuharibika
miundombinu na wengine kucheleweshewa kuungiwa umeme kwa zaidi ya miezi sita .
Post a Comment