Shirika la Internews Tanzania latoa Fundisho kwa Waandishi wa Habari Pemba
WAANDISHI wa habari
Pemba wametakiwa kuandika na kutangaza habari ambazo zitaleta mabadiliko kwa
jamii na kujiepusha na taarifa ambazo zinaweza kusababisha migogoro ya kijamii.
Washiriki wa kikao
hicho wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Mkufunzi Bi. Lakok Mayomb (kulia).
|
Mkufunzi wa habari
kutoka shirika la Internews, Bi Lakok Mayombo ameyasema hayo wakati akizungumza
na wandishi wa Redio Jamii Micheweni, kwenye kikao cha kuwajenga uwezo wa
kuandika habari zenye kuleta mabadiliko.
Amesema ni jukumu
la waandishi kuzifanyia uchunguzi taarifa zao
kabla ya kuzitangaza na kuangalia kama zinaweza kuisaidia jamii pamoja
na mamlaka za kiutawala.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha Redio
Jamii Micheweni, GASPARY CHARLES, akitoa uzoefu wake juu masuala ya uandaaji wa
vipindi katika kikao hicho.
|
Mapema meneja wa Redio
Jamii Micheweni Ali Massoud Kombo amesema Wilaya ya Micheweni imepiga hatua
kubwa kimaendelea tokea kituo cha Redio kianze kufanya kazi
Kikoa hicho ambacho
kiemefanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Redio Jamii Micheweni, ni mwendelezo wa mikutano inayoratibiwa na Shirika hilo
kupitia Mradi wa Boresha Habari, wenye lengo la kuwabadilisha wandishi wa
habari ili kuweza kuandika habari zenye tija katika mabadiliko .
Post a Comment