Wafanya Biashara Soko la Konde waomba Mazungumzo na Serikali kuimarisha Biashara zao
UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
umeshauriwa kuandaa Mazingira mazuri ya kuvihamisha vibanda vya Biashara katika
mji wa Konde na kuvihamishia ndani ya soko la matunda na mboga mboga Konde.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa
soko hilo, Khamis Ali Ngoma amesema uwepo na vibanda vya biashara nje ya soko
hilo , kunaikosesha serikali mapato .
Amesema soko hilo ambalo limejengwa na Serikali na
kugharimu mamilioni ya fedha, kwa sasa biashara ndani yake sio nzuri, huku
akishauri gari la abiria kutoka Chake ziruhusiwe kushisha abira kwenye viwanja
vya soko hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Mhe Shamata Shaame
Khamis amewataka wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na Serikali kwa
kuhakikisha soko hilo linatumika na kuloeta tija.
Amesema ni vyema uongozi wa soko kukaa pamoja na
wafanyabiashara kuzungumzia suala la kuvihamisha vibanda vidogo vidogo na
kuwataka waingie ndani ya soko jambo ambalo litaondoa usumbusu wa ukusanyaji wa
mapato.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
Hamad Mbwana Shehe amesema wafanyabiashara wanaendelea kulitumia soko hilo kwa
ajili ya kuuza biashara zao .
Post a Comment