Maji Chumvi yazidi kuwaathiri Wakulima Pemba, Wasema wasipoangaliwa Njaa itawateketeza
JUMLA
wa Eka Nane katika bonde la Tovuni lililoko Kiungoni zimeathirika na mabadiliko
ya tabia ya Nchi yaliyosababisha maji ya Chumvi kuvamia bonde hilo pamoja
na wadudu waharibifu wa mpunga aina ya Hispa.
Hali
hiyo imesababisha wakulima zaidi ya 50 kupoteza zaidi ya tani 12 za
mpunga kwa msimu huu, jambo ambalo linatishia faamilia hizo kukumbwa na baa la
njaa.
Wakulima
wa bonde hilo wametaja sababu zilizosababisha hali hiyo ni kukosekana kwa tuta
la kudumu kuweza kuhimili maji ya chumvi yasiingine ndani ya bonde la kilimo.
Katibu
wa bonde hilo Hamad Ali Khatib akizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI
amesema wakulima wa eneo hilo wamehamasika kuendeleza kilimo kwa kukubali
kuchangia gharama za ujenzi wa tuta la kuzuia maji ya chumvi kuingia ndani ya
bonde.
Amefahamisha
kuwa juhudi za wakulima zimeshindwa kuzaa matunda kwani nguvu za maji ya bahari
zimeweza kubomoa tuta ambalo limejengwa na wakulima kwa njia ya kienyeji.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bi Maryam Juma Abdalla
amesema Serikali itafanya utafiti wa udongo ili kujua kiasi cha chumvi
kilichopo kwenye udongo wa bode hilo.
Amefahamisha
kwamba , utafiti huo utaweza kutoa majibu sahihi ambayo yatatumiwa na wataalamu
wa kilimo kuweza kuwasaidia wakulima wa bonde hilo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dr Makame Ali Ussi mbali
na kuahidi kuimairisha kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde hilo, pia
amewasitiza wakaulima kuendelea kushirikiana na wataalamu wa sekta ya kilimo
kuendeleza uzalishaji.
Bonde
la Tovuni lenye ukubwa wa eka 85 na linajumla ya wakulima 281 ambalo baadhi ya
maeneo yake yameathirika na maji ya chumvi na kusababisha wakulima kukosa
sehemu za kilimo.
Post a Comment