'Iwapo dhana hizI zitaendelea kutumika uwezekano wa wavuvi kukumbwa na umaskini ni mkubwa'
UHARIBU
wa Mazingira ya bahari unaofanywa na baadhi ya wavuvi wanaotumia dhana
zilizopigwa marufuku umechangia kupungua mazao ya habaharini wakiwemo samaki
katika bahari wa mwambao ya Pemba.
Wakizungumza
na REDIO JAMII MICHEWENI, baadhi ya wavuvi katika bandari ya Wete, wamesema
uvuvi wa kutumia nyavu za kukokota unasababisha kuvurugwa kwa matumbawe ambayo
ni mazalio ya samaki.
Mmoja
wa wavuvi Mohammed Khamis Juma (45) amefahamisha kwamba sekta ya uvuvi huchangia
ajira kwa vijana wengi, na kwamba iwapo dhana hizo zitaendelea kutumia
uwezekano wa wavuvi kukumbwa na umaskini .
Kwa
upande wake Said Kombo (52) amelalamikia tabia ya baadhi ya wavuvi kutumia
uvuvi wa mabomu ambao unakimbiza samaki kutokana na vishindo vinavyotokea
baharini.
Amesema
baadhi ya wakati anaenda kuvua na kurudi bila samaki , licha ya kwamba
anategemea kazi ya uvuvi kuendesha maisha yake pamoja na familia yake
Afisa
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini, kutoka Wizara
Kiimo , Malasili, Mfugo na Uvuvi Pemba Sharif Mohammed Faki amekiri kuwa
uvuvi wa kutumia dhana haramu unasababisha kupungua samaki baharini.
Amesema
, katika kukabiliana na hali hiyo , Idara imekuwa ikiwatumia wajumbe wa kamati
za wavuvi za shehia na Wilaya kuwaelimisha wananchi kuzingatia uvuvi unajali
hifadhi ya mazingira ya bahari.
Akizungumzia
athari za uvuvi huo, Sharif amesema unaathari kubwa kwa viumbe vya baharini,
kwani hukokozoa vyakula vya samaki na kuvunja matumbawe jambo ambalo
linakimbiza samaki na kukimbilia maji makubwa.
Kwa
mujibu wa sheria ya Uvuvi namba 7 /2010 sehemu ya tano na sita , inazungumzia
marufuku ya matumizi ya dhana haramu pamoja na adhabu yake kwa atakayebainika
kuhusika na vitendo hivyo .
Post a Comment