Wazazi, Kamati Micheweni wakubaliana kuhusu upatikanaji wa haki ya Elimu kwa Watoto
WAZAZI
katika Shehia za Tumbe Mashariki na Magharibi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, pamoja na
Walimu wamekubaliana kuweka mikakati ya kupinga udhalilishaji na kuongeza
upatikanaji wa haki ya elimu kwa watoto wao Wilayani hapa.
Hayo
yamejili katika kikao cha Wazazi pamoja na kamati za Skuli cha kutathimini
mpango kazi wa upatikanaji wa haki ya elimu na kupinga udhalilishaji katika
sikuli ya msingi Tumbe kilichoandaliwa na Shirika la SOS Children’s Village
Zanzibar.
Nassor
Rashid Said Mwalimu Mkuu Skuli ya Sekondari Tumbe, akichangia katika kikao
hicho amesema kuwa walimu wanakosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya wazazi na
kupelekea watoto kukosa haki yao ya elimu ambayo husababishwa na utoro.
Massoud
Ali Hamad mmoja wa wazazi akichangi kikaoni hapo amesema kuwa mfumo wa elimu ya
sasa pia nao umekuwa ni chanzo cha watoto wengi kushindwa kupata haki ya elimu
ipasavyo kutokana na kuwa Elimu ya Madrasa waliowengi huikosa.
Akizungumza katika
kikao hicho, Afisa mradi kutoka sirika hilo, Gharib Abdallah Hamad amesema ili watoto waweze kupata haki yao
kielimu ni lazima Wazazi wawe tayari kushirikiana na Walimu kwa kufuatilia
Mwenendo wa Watoto wao.
Awali
akizitaja changamoto zinazopelekea watoto kukosa haki ya elimu, Afisa huyo
amesema ni pamoja na ukosefu wa lishe majumbani hasa kwa watoto wanaosoma skuli
za mbali, usimamizi duni wa wazazi juu ya maendeleo ya skuli kwa watoto.
Post a Comment