Header Ads

WAZIRI: 'Ugatuzi wa Madaraka Zanzibar haujalenga kumuonea Mtu,Taasisi'


WAZIRI wa Kilimo ,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mh Rashid Ali Juma amesema Serikali imetekeleza mpango wa ugatuzi ili kuweza kushusha maendeleo kwa  wananchi pamoja na kuongeza kasi ya utendaji.

 Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo  Weni Wilaya ya Wete   kwenye  mkutano wa wadau kuhusu maeneo ya ugatuzi  katika  Wizara hiyo.

Mhe Rashid amewataka watendaji hao kuacha kulalamika kwamba kugatuliwa ni kuonewa na kuwasisitiza kuongeza uwajibikaji  kwa kutofanya kazi kwa mazoea.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ahmad  Kassim amewataka wafanyakazi walioingia kwenye mpango wa  ugatuzi kutekeleza vyema wajibu wao kwani wanaendelea kuitumikia serikali yao .

Ugatuzi umekuja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi  na kuwataka maafisa ambao wameingia kwenye mpango kufanyakazi kwa mujibu wa sheria .

No comments