Shirika la SOS lawakutanisha wadau wa Elimu, Wazazi Micheweni kujadili maendeleo ya Elimu
WAKAAZI wa Shehia
ya tumbe Mashariki wametakiwa kutoa mashirikiano juu ya upatikanaji wa lishe na
malezi kwa watoto wao ili kuwa na afya bora.
Hayo yamesemwa na
Afisa mradi wa SOS Pemba Gharib Abdallah Hamad wakati akizungumza na wazazi,
walezi pamoja na kamati mbali mbali za maendeleo kwa watoto katika skuli ya
tumbe msingi.
Amesema nivyema
wazazi na walezi kushirikiana kutoa huduma ya lishe na malezi kwa watoto, ili kupunguza watoto hao kujiepusha
na ajira za utotoni.
Kwa upande wa mzazi
Massoud Ali Hamad amesema kwa sasa
wamepiga hatua mbele kwa malezi ya watoto wao na masuala ya vitendo vya
udhalilishaji vimepungua kwa kiasi kikubwa kulingana na kiwango kilicho kuwepo
ndani ya shehia hiyo.
Nae kaimu afisa
elimu wilaya ya micheweni Mwalimu Bakar Khamis amewataka wazazi na walezi
kutokuwa wa kimya kwa watoto wao na kuwaeleza matatizo yanayo jitokeza.
Afisa wanawake na
watoto wilaya ya micheweni Bizume Haji Zume amesema malezi yamekuwa ya watoto
yamekuwa yakielekezwa upande wa mama pekeake na kushindwa kuwahudumia watot
ipaswavyo.
Amewataka wazazi wa
kiume kujua wajibu wao katika familia, kuwa wao ndiwo wasimamizi na viongozi na
kuto kuwaachia majukumu mazito akina mama katika jamii zao
Post a Comment