Waziri SMZ: 'Serikali inaendelea kuandaa mazingira bora yatakayowawezesha wanafunzi kupata Elimu'
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili Mhe Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali
inaendelea kuandaa mazingira bora yatakayowawezesha wanafunzi kupata elimu ili
asiwepo mtoto anakosa elimu.
Amesema
kuwa lengo la serikali ni kuona kila mwanafunzi anatimiza ndoto zake za kupata
elimu bora ambayo itamsaidia katika maisha yake pamoja na familia yake.
Mhe
Aboud ameyasema hayo wakati akungua kituo cha maktaba ya kutumianjia ya umeme
katika skuli ya Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amefahamisha
kwamba kufunguliwa kwa kituo hicho ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuinua
kiwango cha elimu nchini na kuwataka wanafunzi kukitumia kwa ajili ya kungeza
maarifa na uweleza wa masomo yao.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewasisitiza wazazi
kuwapa fursa ya kusoma watoto wa kike na kuacha kuwakatisha masomo na kuolewa.
Amesema
haki ya kupata elimu ni ya wote hivyo wanapaswa kuzingatia kwamba hata mtoto wa
kike anaweza kusoma na kuisaidia jamii yake baada ya kuhitimu elimu yake.
Mwakilishi
wa Jimbo la Micheweni ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa, serikali za mitaa na Idara maalumu za SMZ Mhe Shamata Shaame Khamis
amesema kwa ushirikiano wa wazazi na hjamii ya kiuyu watakituza kituo hicho ili
kiweze kutumika kama ilivyo kusudiwa.
Post a Comment