Kuelekea Mwezi wa lishe na Afya ya Mtoto Pemba, Jamii yashauriwa haya
JAMII imeshauriwa kuendelea
kuzingatia suala la utumiaji wa lishe bora kwa akinamama wajawazito pamoja na
watoto ili kuwawezesha kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali nyemelezi.
Akizungumza na waandishi
wa habari katika uzinduzi wa mwezi wa lishe na Afya ya Mtoto, Mkuu wa kitengo
cha Lishe Pemba, Raya Mkoko Hassan amesema kuwa Wizara ya Afya kupitia kitengo
hicho wanautumia mwezi huu kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo Matone na Dawa
za Minyoo.
Raya amesema kuwa
jamii nyingi zimekuwa hazizingatii ushauri wa kitaalam juu ya ulaji wa mlo
kamili hasa kwa akinamama wajawazito na watoto hivyo kupelekea madhara
mbalimbali ikiwemo Utapiamulo na hata kuharibika kwa baadhi ya mimba.
Awali akichangia
Mratibu wa lishe Wilaya ya Mkoani, Mwajine Khamis Mjaka amevitaka vyombo vya
habari kuendelea kupaza sauti kuwahamasisha wanajamii juu ya umuhimu wa Lishe bora
katika maisha yao.
Waandishi wa habari walioshiriki kikao hicho
wakimsikiliza mkuu wa kitengo cha Lishe
Pemba, Raya Mkoko Hassan akiwasilisha mada
|
Mwajine amesema
kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika baadhi ya maeneo kuhusiana na
zoezi hilo, lakini vyombo vya habari vinalojukumu kubwa kuhakikisha jamii
inapata elimu ya lishe.
Zoezi la utoaji wa chanjo
ya lishe na Afya ya Mtoto Pemba hufanyika kila ifikapo miezi ya June na Desemba
ya kila mwaka ambapo takwimu zinaonesha
kwamba kwa mwaka 2017 zoezi hilo lilifanikiwa zaidi ya 90% .
Post a Comment