ZYF Yawafunza Vijana Micheweni mbinu za upangaji malengo
Almas Mohamed Ali Mratibu wa mradi akitoa mada |
VIJANA wajasiriamali katika
Wilaya ya Micheweni wametakiwa kujenga uthubutu, msukumo na nia ya kufanikiwa
kupitia malengo yao ili kupunguza hisia hasi ambazo ni kikwazo cha maendeleo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo |
Ushauri huo umetolewa katika
mafunzo kwa vijana wa Willaya ya Micheweni na mratibu wa mradi wa
kuwajengea uwezo vijana wa kupanga malengo kwa ajili ya maendeleo (Setting
myself for Success Program), Almas Mohamed Ali kupitia taasisi ya Vijana
Zanzibar (Zanzibar Youth Forum).
Amesema pamoja na changamoto
zinazowakabili vijana, lakini wanapaswa kuwa wajasiri kwa kutokimbia
changamoto bali watumie ubunifu wao kuzigeuza kuwa fursa.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo |
Hata hivyo amewataka vijana
kujitathimini pamoja na kujipenda na kufurahia matokeo ya kazi zao ikiwa
ni sambamba na kukaa karibu na watu waliofanikiwa.
“Vijana wanapaswa kujenga
ujasiri wa kutokimbia changamoto pamoja na kuwa karibu zaidi na waliofanikiwa
ili waweze kuambukizwa njia za mafanikio”alisisitiza.
Khairat Hamad Salim mmoja wa
washiriki kutoka shehia ya Kinowe, amesema bado fursa na rasilimali zilizopo
hazijatumika ipasavyo kuwaendeleza vijana, kutokana na mawazo mgando kwa
baadhi yao kutegemea ajira kutoka serikalini.
Mmoja wa washiriki Abdalla akichangia katia mafunzo hayo |
Mjumbe wa baraza la Vijana
Wilaya hiyo Abdalla Khamis Shaame amesema kupitia mabaraza ya vijana, vijana
wamekuwa wakishajihishwa kuwa wajasiriamali lakini changamoto kubwa ni ukosefu
wa elimu ya ujasiriamali.
“Ujio wa mafunzo haya
yatatusaidia sana katika uendelezaji wa shughuli zetu kwani vijana wengi
kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali wamekuwa wakikata tama mapema pale
wanapokumbana na changamoto katika kazi zao,” alisema.
Mafunzo hayo ya siku Tatu
yaliyoandaliwa na taasisi ya Jukwaa la Vijana Zanzibar (Zanzibar Youth Forum
ZYF) ya kuwajengea uwezo Vijana wa kupanga malengo kwaajili ya maendeleo yao kupitia ufadhili wa taasisi ya The foundation for Civil Society, yamewashirikisha vijana
zaidi ya 20 kutoka Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
PICHA NA GASPARY CHARLES- MICHEWENI FM |
Post a Comment