Kilele Maonyesho SABA SABA: Rais Mwinyi Awaonesha Wajasiriamali Milango ya Fursa Soko la AFRIKA
DAR-ES-SALAAM
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ZANZIBAR MHE DKT HUSEIN ALI MWINYI AMEWATAKA WAZALISHAJI NCHINI KUONGEZA UZALISHAJI WA BIDHAA ILI KUCHANGAMKIA SOKO LA AFRIKA, NA MAENEO MENGINE DUNIANI.
RAIS MWINYI AMETOA RAI HIYO WAKATI AKIHITIMISHA MAONYESHO YA 47 YA BIASHARA YA YA KIMATAIFA DAR-ES-SALAAM MAARUFU SABASABA.
AMESEMA TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI NANE ZA AFRIKA ZILIZORIDHIA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA NCHI ZA AFRIKA HIVYO WAZALISHAJI NCHINI HAWANA BUDI KUONGEZA UZALISHAJI HASA WA MALIGHAFI ZA NDANI WA BIDHAA KAMA VILE KAHAWA , SUKALI NA NAFAKA NA KUZIELEKEZA KWENYE MASOKO YA KIKANDA AFRIKA IKIWEMO UKANDA WA SADC.
AIDHA RAIS MWINYI AMESEMA MAONYESHO YA BIASHARA YA ADAR-ES-SALAAM YANAFANYIKA SAMBAMBA NA UFUNGUAJI WA MASOKO NA KUONGEZA UWEKEZAJI, NA AMEZISHUKURU WIZARA ZA VIWANDA NA BIASHARA ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KWA USHIRIKIANO WAO.
NAYE WAZIRI WA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA ZANZIBAR MHE OMAR SAID SHAABAN AMESEMA SERIKALI YA MUUNGANO NA YA MAPINDUZI ZANZIBAR ZINAENDELEA KUHAKIKISHA KUWA SEKTA BINAFSI AMBAO NI WADAU WAKUU WA UIMARISHAJI BIASHARA NA UWEKEZAJI INAIMARIKA.
MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANTRADE BI LATIFA MOHAMED KHAMIS KUMEKUWEPO NA MAFANIKIO ZAIDI KWENYE MAONYESHO YA MWAKA HUU NA KUONGEZAKA KWA NCHI KADHAA KATIKA USHIRIKI WA MWAKA HUU.
MAPEMA
MARA BAADA YA KUWASILI KWENYE MAONYESHO HAYO RAIS MWINYI AMBAYE ALIAMBATANA NA
MKEWE MAMA MARIAM MWINYI ALITEMBELEA MABANDA KADHAA LIKIWEMO BANDA LA ZANZIBAR,
BANDA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI, BENKI YA WATU WA ZANZIBAR , NA JKT
Post a Comment