OTHMAN MASOUD: SERIKALI KAZI YAKE NI KUCHUKUA KODI TU, LAKINI WATU WANACHUKUA ARDHI WANAUZA WAO
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba Zanzibar inahitaji kuwepo mfumo na utaratibu bora wa matumizi na usimamizi sahihi wa ardhi ili kuwawezesha wananchihi kufaidika vyema na rasilimali hiyo ili waweze kupambana vyema na umasikini.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko
Mkwajuni wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja alipohutubia wananchi na wafuasi wa chama hicho katika mkutano
wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa mikutano mbali mbali ya ACT - Wazalendo
inayoendelea katika mikoa mbali mbali Unguja na Pemba.
Aidha amefahamisha kwamba iwapo
serikali itakuwa na mfumo bora na sahihi utasaidia wananchi wanaomiliki rasilimali hiyo kupata kipato
kikubwa zaidi kutokana na ukodishaji, huku serikali nayo ikaweza kufaidika
katika kusanyaji wa kodi inayotokana na aradhi
hiyo.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amefahamisha
kwamba ardhi ni rasilimali muhimu ya umma ambayo mwananchi anayemiliki
anahitaji kuwezeshwa kwa kuandaliwa
utaratibu bora utakaleta tija na faida kubwa kupitia uwekezaji wa aina mbali mbali unaofanywa
na wawekezaji wa ndani nba nje ya nchi.
Aidha amefahamisha kwamba utaratibu
uliopo sasa hauna tija na manufaa makubwa kwa wananchi ambao ardhi zao
zinatumika kwa uwekezaji jambo ambalo linachangia kutofanikiwa katika kupambana
na umasikini.
Mhe. Othman amesema kwamba sera
bora na mipango mizuri ya usimamizi wa rasilimali hiyo ni njia sahihi ya kumuezesha
mwananchi wa kawaida kuweza kupata kipato kikubwa zaidi na kujikwamua na tatizo la umasikini
kama zinavyofanya nchi mbali mbali duniani.
Mhe. Othman amesema kwamba hatua
hiyo ni muhimu kwani itasaidia sana
katika jitihada za ujenzi wa Zanzibar
mpya ambayo itawafanya wananchi kuondokana na tatizo la umasikini sambamba na
kudumisha , umoja Amani na mshikamano wa kweli.
Amesema kwamba ni muhimu
kuzingatiwa kwa suala hilo kwani uchumi ,
maendeleo bora na amani ya kweli katika nchi yoyote duniani yanatokana
na wananchi kuwa na mamlaka ya kamili ya kuwachagua na kuwawajibisha viongozi
wao katika ngazi mbali mbali.
Akizungunzia suala la Muungano,
Mhe. Othman amesema kwamba ni muhimu kuwepo Mungano wenye mkataba madhubuti unaotoa na kusimamia maslahi yenye uwiano sawa
kwa pande mbili za muungano ili taija ya suala
hilo iweze kupatikana na kuwafaidisha wote.
Mhe. Othman amewata wananchi na
wafuasi wa chama hicho kuendelea kuinunga mkono ACT- ili kiweza kuwa na uwezo na mamlaka ya kusimamia ipasavyo
maslahi ya Zanzibar na kuchangia maendeleo ya wananchi katika nyanya mbali
mbali.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Ismali Jussa Ladhu, amesema nchi
haiwezi kupiga hatua na kuwa na maendeleo iwapo hakutomkuepo na jitihada za kupinga vitendo vya ufisadi hasa katika taasisi za serikali nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome
ya Wanawake Taifa ya Chama hicho Pavu Juma Abdalla, amesema kwamba utaratibu
usiofaa wa usimamizi wa ardhi unachangia sana kuwafanya wanawake wa Zanzibar kuwa
ndio waathirika wakubwa wa masuala hayo hasa kwa vile wao ndio wakulima wakubwa
wanaosaidia familia kupitia juhudi za kilimo cha aina mbali mbali.
Mapema Mhe. Othman alifika huko Donge Muwanda Kuifariji familia ya Bwana Mohammed aliyefiwa na watoto watatu hivi karibuni kwa kuzama kwenye mashimo yenye maji, na pia Donge Kipange na kutembelea kuwapa pole wagonjwa na wafiwa katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja .
Post a Comment