ELIMU YA DEMOKRASIA KUTOKA SHIRIKA LA ACTIONAID YAWAFUNGUA VIJANA PEMBA
VIJANA wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wametakiwa kujua mkataba wa Afirika Mashariki kuhusiana na Demokrasia, Utawala Bora na haki za Binaadamu katika Taifa lao.
Ushauri huo umetolewa na MWANAID ALI SAID Kutoka
shirika la ACTION AID wakati alipokuwa akifunga
mafunzo ya siku mbili juu ya Demokrasia, Utawala Bora na haki za Binaadamu katika ukumbi wa Jamhuri Wete.
Amesema kuwa wameamua kuwasaidia vijana kwa kuwapatia
mafunzo yademokrasia,utawala bora na haki za binaadamu ili kuweza kujua wajibu wao ndani ya serikali
na jamii kwa ujumla.
Akizungmza katika mafunzo hayo mjumbe kutoka shirika
la umoja wa Mataifa UN, Mohamed Hassan Ali amesema vijana wakijuwa demokrasia
na haki za binaadamu taifa linaweza kupiga hatuan za kimaendeleo
Ali amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya vijana
ambao wanajiingiza katika masuala la kisiasa kutokana na wengi wao kutokuwa na
elimu ya kutosha juu ya siasa.
Nao baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo hayo
wamesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata kutoka shirika hilo yamewasaidia
kutambua wajibu na mchango wao katika Taifa.
Wamesema mafunzo hayo yamekuja kuwapatia uelewa
wakutosha juu ya kujuwa wazalendo katika taifa lao na kuweza kutowa elimu kwa
vijana wezao ili kuweza kuondosha changamoto ambazo zinzweza kuwatokiea
Post a Comment