ASHIKILIWA NA ZAECA AKITUHUMIWA KUTOA RUSHWA YA SHILINGI LAKI MOJA.
Pemba.
Mohammed
Said Mohammed (46)
mkaazi wa Ngwachani anashikiliwa na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu
wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) Mkoa wa Kusini Pemba akituhumiwa kutoa rushwa ya shilingi
laki moja ili kumshawishi mwananchi kuficha taarifa ya mashamba ya Serikali
ambayo mtuhumiwa anayamiliki kinyume na taratibu.
Mtuhumiwa
huyo amekamatwa na Mamlaka hiyo akidaiwa kutoa rushwa na shilingi laki moja kwa
mwananchi (jina limehifadhiwa) ili asitoe taarifa ya mashamba ya Serikali
ambayo mtuhumiwa anayamiliki kinyume na taratibu.
Akizungumza
na blog hii , Mkuu wa Mamlaka hiyo Mkoa wa Kusini Pemba Suleiman Ame amesema
walipokea taarifa kwa mwananchi huyo akidai kuahidiwa kupewa fedha kiasi cha
laki moja ili amsaidie mtuhumiwa kuyaficha mashamba ya Serikali .
Amesema
uamuzi wa mtuhumiwa huyo kutaka kutoa rushwa , umetokana na Serikali kuendesha
zoezi la uhakiki
wa mashamba yake ili kuyakodisha ambapo baadhi ya mashamba ambayo yalikuwa
katika zoezi la kukodishwa yanatumiwa na mtuhumiwa .
“Ni
kweli tunamshikilia mtuhumiwa Mohammed Said Mohammed wa Ngwachani kwa tuhuma za
kutoa rushwa ya shilingi laki moja ili afiche taarifa za mashamba ya
Serikali ambayo anayatumia kinyume na taratibu ”alifahamisha.
Amesema
kuwa Mamlaka itaendelea kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na wananchi
wanaohujumu uchumi wa nchi ili kudhibiti mapato ya Taifa .
Aidha
amewataka wananchi kushirikiana na Mamlaka katika kufanikisha udhibiti wa
vitendo vya utoaji na upokeaji wa rushwa kwa maslahi ya nchi .
“Tunaomba
sana wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa
Uchumi (ZAECA) ili kufanikisha udhibiti wa vitendo vya uhujumu wa uchumi
”alisisitiza.
Mtuhumiwa
huyo anaendelea kuhojiwa na Mamlaka na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinamkabili upelelezi utakapo kamilika.
Post a Comment