ELIMU INAHITAJIKA KUTOLEWA KWA WAFUGAJI WA MBWA KISIWANI PEMBA
Pemba.
IDARA ya Maendeleo
ya Mifugo Kisiwani Pemba imesema uwepo wa mbwa wasiokuwa na wenyewe , wanachangia
kuwepo na ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa baadhi ya maeneo ya kisiwani hicho.
Afisa Mkuu wa
Idara hiyo Asha Zahran Mohammed amesema wafugaji wa mbwa wa Wilaya ya Micheweni na Chake Chake bado wanahitaji
kuelimishwa zaidi ili waweze kujitokeza na kuwapeleka mbwa wao kupata chanjo.
Amesema
kuwa asilimia kubwa ya mbwa wanaofugwa Idara imewapatia chanjo , lakini
kinachoenekana kuwa ni kikwazo na uwepo wa idadi kubwa ya mbwa
waliokuwa na wenyewe .
Akizungumza
na blog hii Asha amesema mbwa ambao
hawana wenyewe hususani katika Shehia ya Kiuyu Mbuyuni kuna idadi kubwa ya mbwa
wasiofugwa , ambao wananchi hawawezi kuwadhibiti.
Amefahamisha
kwamba hata wakati za zoezi la kuchanja mbwa lililofanyika mwezi septemba mwaka
jana , hakukuwa na mwitikio mzuri wa wafugaji wa mbwa wa shehia hiyo jambo ambalo linapelekea shehia hiyo kuendelea
kuripotiwa kesi za watu kung’atwa na mbwa.
“Wilaya ya
Micheweni hususani Shehia ya Kiuyu Mbuyuni bado kesi za watu kungatwa na mbwa zinaedelea
kuripotiwa , kwani hata wakati wa chanjo iliyofanyika mwaka jana hakukuwa na
mwitikio mzuri wa wafugaji wa mbwa kuwapeleka kupata chanjo ”alieleza.
Mkuu wa Mkoa
wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amewataka wananchi wa Wilaya ya Micheweni kutambua
kwamba kichaa cha mbwa ni hatari na ni balaa ambayo ikitokea haimpati mtu mmoja
.
Amesema ni vyema wafugaji wa mbwa kushirikiana na
wataalamu wakati wa zoezi la kuwachanja mbwa ili kuwakinga kupata ugonjwa wa
kichaa ambao ni hatari pia kwa maisha ya binadamu .
“Ni vyema
wananchi wa Wilaya ya Micheweni kutambua kwamba kichaa cha mbwa ni ugonjwa
hatari na ambao unaweza kumpata mfugaji na asiye kuwa mfugaji , hivyo ni vyema
wananchi wanaofuga mbwa kuhakikisha mbwa wao wanawapeleka kupata chanjo ”alisisitiza
.
Aidha amewazitaka
taasisi zinazoendesja zoezi la kuwachanja mbwa kutoa maelekezo kwa Serikali ya
Mkoa sehemu ambazo wanapatikana mbwa wasiofugwa ili waweze kuangamizwa .
Idara ya
Maendeleo ya mifugo Pemba inatarajia kufanya kampeni ya kuchanja mbwa wote ili
kuwakinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa mwezi disemba mwaka huu , ambapo
maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika .
Post a Comment