WALIMU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA UFANISI ILI KUONGEZA UFAULU.
PEMBA.
MWAKILISHI
wa Jimbo la Gando Mhe Mariam Thani Juma ameutaka Uongozi wa Skuli ya Sekondari
Kizimbani kufanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi
katika skuli hiyo.
Amesema kuwa
ni vyema kamati ya skuli kuwasimamia walimu na kuhakikisha wanaingia na kutoka darasani kwa mujibu wa muda uliopangwa.
Akitoa msaada
wa vifaa vya ujenzi ili kukamilisha jengo la Skuli hiyio Mhe Mariam amesema uongozi
wa Skuli hiyo unajukumu la kuhakikisha msaada huo unatumika kama
ulivyokusudiwa.
Nao Uongozi
wa Skuli hiyo umempongeza mwakilishi huyo kwa msaada wake wa kumalizia jengo la
madarasa matatu kwa hatua ya kuezekwa na unyanyuaji wa ukuta wa jengo hilo.
Msadizi Mwalimu
Mkuu wa Skuli hiyo Omar Hamad akizungumza kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Skuli
hiyo amemuomba mwakilishi huyo kuendelea kupeleka huduma za kijamii kama wajibu
wake bila ya upendeleo.
Post a Comment