MWALIM APIGWA AKIWA DARASANI.
PEMBA
MWALIMU mmoja wa skuli ya sekondari
ya Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Khamis Juma ‘masta’ amedaiwa kupigwa
na mzazi akiwa darasani anasomesha skulini hapo.
Ilidaiwa
mzazi huyo awali alifika ofisi ya Mwalimu mkuu kumuuliza mwalimu huyo, huku
akiwa na tabasabu na ndipo alipoelekezwa kuwa mwalimu huyo yuko darasani
akiendelea kuwafundisha watoto.
Mara baada
ya mzazi huyo alietambulika kwa jina la Salim Ussi Shaame “zinga’ kumfika
mwalimu huyo, alimueleza kuwa alipata ujumbe kutoka kwa mwanawe kwamba anamuita
skulini hapo, ingawa mwalimu alijibu kuwa yeye hakumbuki hilo.
Aidha
taarifa zinaeleza kuwa, mara baada ya mwalimu huyo, kumfahamisha mzazi huyo
kwenda ofisi ya Mwalimu mkuu, alivamia darasani na kumkunja mwalimu huyo kwa kipigo.
Mwalimu Mkuu
wa skuli hiyo Ridhiwani Haji Makame, alisema wakati mzazi huyo akiwa amemkunja
mazazi huyo, ndipo alipoanza kumkunja na kumshambulia kwa vibao huku akitamka
kuwa amemjibu jeuri.
“Mzazi
wakati anampiga mwalimu huyo akiwa darasani, anadai kuwa amejibiwa jeuri na kwa
kule kuelezwa kuwa aende ofisi ha Mwalimu mkuu ili kusikiliza
wito’’,alifafanua.
Aidha
Mwalimu mkuu huyo, alisema mwalimu huyo hata ilipofika hatua ya kupapatuliwa
alichirika damu za mdogo baada ya kupasuka kwa kushambuliwa na mzazi huyo.
Kufuatia
tukio tayari uongozi wa skuli hiyo, ulikutana ghafla na kwenda kituo cha Polisi
kwa ajili ya kuchukua fomu ya matibabu Ff3, na kisha kwenda hospitali kwa
matibabu.
Mwenyekiti
wa kamati ya skuli hiyo Abdalla Salim Juma, alisema tukio hilo limetokwa majira
ya saa 3:15 wakati mwalimu huyo, akiendelea na kazi yake ya kusomesha.
Alisema yeye
alikuwa kwenye safari yake ya kawaida skulini hapo na kuikuta kesi hiyo, ambapo
ghafla aliitisha kikao na waalimu juu ya tukio hilo.
“Baada ya
kutokezea hali, hiyo sisi kwanza tuliilani lakini kishwa Mwalimu mkuu
aliongozana na mwalimu aliepigwa hadi kituo cha Polisi kwa ajili ya taratibu
nyengine”,alifafanua.
Chanzo cha
tukio kinaelezwa kuwa mtoto wa mzazi huyo pamoja na wengine sita, walifika
skuli hapo kama kawaida wakiwa wamevaa flana zisizokubalika ingawa, watano
walitii amri ya kuzivua.
Ilifahamika
kuwa, mwanafunzi huyo baada ya kushindwa kutii, agizo hilo alitakiwa arudi
nyumbani na kurujea skuli hapo, akiwa na mzazi wake.
Ingawa baada
ya mzazi huyo kufika skuli hapo, akiwa hali ya kawaida na kumuulizia mwalimu
huyo, ambae sie miongoni mwa waalimu waliotoa agizo hilo na kujitokeza hali
hiyo.
Mwalimu
aliedaiwa kupigwa na mzazi huyo Mohamed Juma Khamis ‘masata’ alisema hakubuki
kumjibu jeri mzazi huyo, bali alishangaa baada ya kumuelekeza kwenda ofisi ya
Mwaliku mkuu kwa ajili ya kuitikia wito.
Alieleza
kuwa, laiti kama sio kutokezea msamaria mwema alieskia zogo na kumpapatua mzazi
huyo engelimuumiza vibaya, kutokana na vibao alivyokuwa akimpiga.
“Mimi sikumbuki
kuwa mimi na yeye tunaugomvi wowote, naona alinivamia tu na kunipiga vibao na
mimi kunipasua mdomo na kutoka damu”,alisema.
Hadi jana
bado mtuhumiwa huyo hajakamatwa na Jeshi la Polisi, ingawa tayari barua
imeshatumwa kwa sheha wa shehia ya Chumbageni ili kumfikishia.
Hili ni
tukio la pili kwa mwaka huu, kwa mwalimu kupigwa na mzazi akiwa darasani,
ambapo mara ya kwanza lilitokea skuli ya Michenzani Mkoani.
Post a Comment