JUMUIYA ZA UFUGAJI WA NYUKI KISIWANI PEMBA ZATAKIWA KUFANYA UADILIFU NA KUWA WAVUMILIVU ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KAZI HIYO.
Pemba
Viongozi wa jumuiya ya wafugaji
nyuki Kisiwani Pemba (JUWANPE) wametakiwa kuwa waadilifu na wavumilivu katika
kukabiliana na changamoto za utendaji wa
kazi zao ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndani ya jumuia hiyo.
Wito huo umetolewa na Afisa mipango
Wilaya ya Chake Maalim Kassimu Ali Omar katika mkutano wa uchaguzi wa viongozi
wapya JUWANPE huko katika kituo cha wafugaji nyuki Chake chake Kisiwani Pemba.
Maalim Kasimu amesema uongozi ni
taaluma hivyo viongozi hao hawana budi kufuatilia shughuli za wanachama wao na
kuwaunganisha pamoja ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni
Mwenyekiti wa Mwanvuli wa jumuiya za kiraia Kisiwani Pemba (PACSO) Maalim Omar
Ali Omar amesisitiza haja ya kudumisha umoja na mshikamano walionao ili kujenga
ufanisi wa ufugaji na uzalishaji asali kwa wanachama wa jumuiya hiyo.
Katika uchaguzi huo Ndugu Kmamis
Suleiman Massoud alichagauliwa kuwa Mwenyekiti , Othman Bakar Shehe kuwa Makamo
na Shaibu Haji Zubeir kuwa katibu.
Wengine ni Bi Andikalo KHAMIS Juma
msadizi katibu ,Moza Khamis Abdalla Mshika Fedha na Shehe Matar Shehe kuwa
Msaidizi Mshika Fedha ambao pamoja na wajumbe wengine watano watakaoingoza
jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka minne ijayo,
Akitoa shukurani mwenyekiti mpya wa
Jumuiya hiyo Khamis Suleimani Massoud amesema pamoja na viongozi wengine
watakuwa kitu kimoja katika kulifikia lengo la kuundwa jumuiya hiyo.
Post a Comment