MAMLAKA YA MAJI WILAYA YA ICHEWENI YAWATAKA WANANCHI KUTUNZA NA KUENZI VYANZO VYA MAJI
PEMBA
Mamlaka
ya maji wilaya ya micheweni imewataka wananchi wanaonufaika na huduma ya maji
safi na salama kuyatunza na kuyaenzi
huku ikiahidi kuwapatia maji safi na salama.
Kauli hiyo imetolewa na
Afisa wa baishara wa mamlaka ya maji wilaya
ya Micheweni Yussuf Ali Faki huko ofisini kwake kilindini mapofu katika shehia
ya Mapofu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema kuwa Mamlaka ya
maji Wilaya ya Micheweni ipo mbioni kuondosha usumbufu wa mgao wa maji kwa lengo la kuondoa kero zinazowakabili baadhi ya wananchi katika vijiji tofauti.
Amevitaja vijiji hivyo
kuwa ni pamoja na Kiuyu Mbuyuni, Mjini
Wingwi, Kwale, Maziwa Ngo,ombe,
Micheweni mjini pamoja na Chamboni. Huku
akisema kuwa tatizo hilo linasababishwa na uchache wa vianzio vya maji.
Aidha amesema kuwa
tatizo la vianzio vya maji na uchakavu wa mitandao ya maji linasumbua, huku
akisema kuwa mamlaka ya maji iko mbioni kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kwa
kuongeza visima vya maji, jambo ambalo litapelekea kuondoka kwa kadhia hiyo.
Ameongeza kuwa baadhi ya wakati mwengine mgao wa maji husababishwa na upasukaji wa mabomba ya kusambazia maji.
Wakati huohuo amewataka
wananchi kulipia maji kwa hiari na kwa
wakati hususan wenye kuingiziwa mifereji majumbani mwao ili kuepusha
usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa ni
pamoja na kukatiwa huduma hiyo.
Sambamba na hayo,
amesema amefurahishwa kutokana na kuongezeka idadi kubwa ya 80% ya watu wanao nufaika na maji safi na salama,
Hali ambayo inawafanya kuongeza juhudi na kuboresha huduma hiyo mijini na vijijini.
Post a Comment