RAIA WANNE WA KENYA WAKAMATWA NA KIKOSI MAALUM CHA KUZUIA MAGENDO KMKM WAKIWA NA MAGUNIA 20 YA NAZI
Pemba
RAIA
wanne wa Kenya wamekamatwa na kikosi Maalumu cha KMKM Kamandi ya Pemba wakiwa
na magunia ishirini (20) ya nazi ambazo walikuwa wakiingiza nchini bila
ya kufuata taratibu za kulipa kodi .
Akizungumza Oifisini
Kwake Wete , Kaim wa Kamanda wa KMKM Kamandi ya Pemba , Luteni Kamanda Hassan
Hossein Ali amesema wakenya hao wametiwa mikononi na KMKM katika bandari ya
Kichungwani Ungi Shehia ya Msuka Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema Mzigo huo
ulikuwa ndani ya chombo kinachofahamika kwa jina la Mdodoki kikiwa hakina
namba za usajili ambacho kilikuwa na mabaharia watano wanne ni Raia wa
Kenya na Mmoja ni Mtanzania ambaye anaishi Mkoa wa Tanga.
Kaimu Kamanda wa KMKM
Pemba ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni wa kikosi hicho amesema kuwa
katika tukio hilo pia wamekamata marobota kumi na moja ya nguo za vitambaa
ambayo nayo yalikuwa yanaingia nchini bila ya kulipiwa ushuru.
Mmoja wa Mabaharia hao
Mohammed Mwasemi Asiran ameeleza kwamba walilazimika kutia nanga katika bandari
hiyo baada ya chombo chao kuharibika jambo ambalo pia liliwalazimu kuutosa
baharini baadhi ya mzigo wao.
Amesema mzigo huo
walikuwa wanaupeleka katika soko la Qatar lililoko Wilaya ya Chake Chake
Mkoa wa Kusuni Pemba na kukiri kwamba walikuwa bado hawajafuata taratibu
kisheria .
Amesema wakiwa ndani ya
chombo kuelekea katika bandari ya Wesha , chombo chao kiliharibika na
kulazimika kutia nanga katika bandari ya Kichungwani ili kuhami usalama wa
maisha yao na kujikuta wakiwa chini ya ulinzi wa KMKM.
Ameongeza kwamba baada
ya kuharibikiwa na chombo walilazimika kuipunguza mizigo yao kwa kuitosa
baharini ili kunusuru usalama wa maisha yao ambapo jumla ya magunia tisa ya
nazi waliyatosa baharini
Mabaharia wengine
ambao wamekamatwa na KMKM ni Hassan Omar Koja 58, Othman Omar koja 33,
Omar Bakar 45 wote ni Raia wa Kenya pamoja na Mussa Omar Ambulue 75 Mkaazi Mkoa
wa Tanga
Post a Comment