WAONGOZA MAGARI YA NG'OMBE PAMOJA NA PUNDA WATAKIWA KUWA NA LESENI
PEMBA
Waongoza magari ya Ng’ombe na Punda wametakiwa kuwa na leseni
wakiwa katika shughuli zao za kupakia mizigo ili kuondoa usumbufu ambao unaweza
kujitokeza katika shughuli zao
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa kaskazini pemba Mbaruku Hassani
Khamis wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya micheweni
kuhusiana na watu ambao wanaendesha gari hizo bila ya kuwa na leseni.
Amesema gari hizo zinatambuliki kisheria kwa mujibu ya sheria
ya 1967 sheria ya usalama barabarani ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 1977
na kanuni na sheria namba 7 ya mwaka
2003 ya usafiri barabarani inaitambua sheria ya magari ya ngombe ,punda pamoja
na mikokoteni
Afandi Mbarouk amesema wanatowa elimu juu ya watumiaji wa
magari hayo ili kuweza kutumia barabara bila kuwa na matatizo ya aina yeyote.
“tunatowa elimu juu ya magari ya ng’ombe na punda kwani
wananchi walio wengi wanatumia usafiri
huo kwa kubebea mizigo bila ya kujua kama magazi hayo yanatakiwa kuwa na leseni”amesema
afande mbaruk
Hata hivyo mkuu wa usalama barabarani wilaya ya wete Ali
Ahmed amesema wananchi katika maeneo ya wilaya wete wameanza kufanyia
kazi elimu waliyoipata juu ya kukata
leseni ya magari ya punda na magari ya ng’ombe
Amesema wameamua kuongeza nguvu katika wilaya ya micheweni ili
na wananchi wa wilaya hiyo waweze
kuipata elimu hiyo na kuanza kuifanyia kazi kwa kukata leseni za magari hayo
ambayo yanatambulika kisheria
“tutaendelea kutoa
elimu na kusimamia sheria kwa wananchi ili jamii iwe na muamko wa kujua sheria
zao “alisema afande ali
Nao wananchi waliokuwa wakipatiwa mafunzo hayo wamesema wamefurahishwa na kitendo cha jeshi la polisi
kutoa elimu juu ya kuwatumikisha wanyama katika jamii yao.
Wamesema jeshi la polisi litakapoendelea kutoa elimu hiyo
jamii itaweza kuelimika na kuweza
kuzitumia barabara ipavyo na kuepukana na ajali zinazojitokeza mara kwa mara katika barabara
zao.
Post a Comment