ELIMU YA UFUGAJI INAHITAJIKA KWA WAFUGAJI WA SHEHIA YA VITONGOJI
PEMBA
BAADHI ya
wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake kisiwani
Pemba, wamesema hawajui njia ya kupita, ili kufikia maendeleo ya ufugaji kama
wenzaao walivyo, shehiani humo.
Walisema wamekuwa wakiwashuhudiwa wenzao wakipewa misaada,
elimu, kuitwa mjini kuhudhuria mafunzo na kutembelewa ingawa wao bado hawajui
njia wenzao waliopita hadi kufikia hatrua hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa blogi hii, wafugaji hao
waliojikusanya kundi la watu watatu wakiwa na Ng’ombe zaidi ya wanne, walisema
na wao wanatamani kufikia maendeleo lakini hawajui chochcoro ya kupita.
Walisema wanapowafuatilia wenzao hawawapi ukweli wa mambo, na
huwaeleza kwamba wasubiri na wajikusanye pamoja, ingawa wao wanaendelea kula
raha kupitia sekta ya ufugaji.
Kiongozi wa muda wa wafugaji hao Abdalla Khamis Abdalla,
alisema Ng’ombe wao aliezaa hivi karibuni amekumbwa na ungojiwa wakuvimba
kiwele na hawajui wapi wampate daktari.
Kiongozi huyo, alisema wanapotafuta ushauri kwa wenzao hukosa
ushirikiano wa kweli, jambo ambalo kinawarejesha nyuma katika kufikia
maendeleo.
“Mi sijui wapi panaposajiliwa vikundu vya ufugaji, hata sheha
hajatwambia juu ya hili, na hawa wafugaji wenzetu wanaopata ufadhili hata wa
kupewa dawa, wamekuwa wazito kutuelekeza”,alifafanua.
Hata hivyo wafugaji hao wamekubali ushauri wa waandishi wa
blog hii, kwamba waachane ne kuwafuata wafugaji wenzao, na badala yake kumfika
sheha wa shehia yao, ili kupata utaratibu.
Nae Salim Ali Said, alisema wamekijikusanya tu pamoja, lakini
hawajajua nini wafanye, maana hawana muongozo wowote wa namna ya kufuga na
kutafuta soko.
“Kwa sasa tunakamua maziwa Ng’ombe wawili, lakini maziwa
tunayauza kwa shilingi kati ya 800 au shilingi 900 kwa lita moja, lakini
tutafuata ushauri wenu”,alifafanua.
Mwenyekiti wa kikundi cha ‘Tumaini’ kinachojishughulisha pia na ufugaji, Mohamed Abdalla Khamis ‘song’
alisema wafugaji hao wamekuwa wazito kufuata taratibu kama tunavyowaelekeza.
“Sisi hawa ni jirani zetu, lakini wao na wengine wanadhani
mkiunda kikundi tu siku ya pili, ndio maendeleo yanamiminika, sasa ni wazito au
hawajafahamu nini maana ya kujitolea”,alieleza.
Sheha wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake Ayoub Salim
Suleiman, aliwataka wafugaji hao kumfika mara moja, ili kuwapa barua ya
uthibitisho na kufuatilia taratibu za uanzishwaji wa kikundi cha ufugaji.
“Mimi hapa ofisini kwangu sisajili kikundi kiwe cha wafugaji,
mboga, hisa au michezo lakini wananchi wakishajikusanya basi waje haraka
niwaelekeze”,alifafanua.
Katika hatua yengine
Sheha huyo, alisema maendeleo ya mtu mmoja mmoja, ni vigumu kufikia na nia
inayotumiwa sasa na wananchi ni kujikusanya pamoja.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walioamua kujikusanya pamoja
kwa shughuli mbali mbali kama za kilimo, ufugaji na kuweka na kukopa, walisema
tatizo linalowakumba waliowengi ni kukosa umadhubuti.
Maryam Saleh Juma Mwenyekiti wa kikundi cha Hisa cha ‘wema
haozi’ alisema kama hakuna kuaminiana na umakini wa hali ya juu, vikundi kadhaa
vitanzishwa bila ya kufikia lengo.
Post a Comment