SERIKALI YA MKOA YAAHIDI KUWACHUKULIA HATUA WANAOSAFIRISHA KARAFUU BILA KUFATA TARATIBU ZA KISHERIA
PEMBA .
Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mhe Omar Khamis Othman amesema
hakuna mwananchi ambaye atasalimika iwapo atakwenda kinyume na sheria kwa
kusafirisha karafuu kutoka shehia moja kwenda nyengine bila ya kuwa
na kibali.
Amesema kwa mujibu wa sheria ya karafuu ni kosa kusafirisha karafuu
kutoka shehia moja kwenda nyengine bila ya kuwa na kibali ambacho kinatambulika
kisheria na ambacho kitatolewa na sheha.
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo baada ya vyombo vya ulinzi kufanikiwa
kumkamata kijana Mbarouk Salim Bakar ambaye alikuwa anasafirisha karafuu
kutoka wilaya ya wete kwenda chake chake bila ya kuwa na kibali.
Mapema mkuu wa wilaya ya wete Rashid Hadid Rashid amesema kijana huyo
amekamatwa baada ya kukaidi agizo la kukata kibali kutoka kwa sheha ambaye
alimtaka afanye hivyo ili kuiwezesha serikali kudhibiti upotevu wa karafuu.
Naye kamanda wa
polisi mkoa wa kaskazini pemba kamishna msaidizi Haji Khamis Haji amesema
wamejipanga kuanza na kijana huyo kwani amefanya kosa kwa mujibu wa sheria ya
karafuu.
Katika utetezi wake kijana huyo amesema alikuwa amepanga kukata cheti
shehia nyengine kwani sheha wa shehia ya piki amekuwa akimlazimisha kuuza
karafuu kwenye vituo vya zstc wilaya hiyo na sio wilaya nyengine.
Post a Comment