Header Ads

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KASKAZINI PEMBA YAENDELEA KUPAMBANA NA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA



PEMBA ..

KIJANA ALI OMAR FAKI  MKAAZI WA CHASASA WILAYA YA WETE AMEKAMATWA NA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KASKAZINI PEMBA AKIWA NA MAJANI MAKAVU YANAYOSADIKIWA NI BANGI NYONGO 26 NA KUKIRI KWAMBA YEYE NI MTUMIAJI WA BANGI .

KIJANA HUYO AMEKAMATWA NA VYOMBO VYA ULINZI ENEO YA SENGENYA SHEHIA YA MTAMBWE KASKAZINI , AMBAPO BANGI HIYO  ALIKUWA AMEIHIFADHI NDANI YA BUTI YA VESPA .

AKIZUNGUMZA  MBELE YA MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KIJANA HUYO  AMETOA SABABU ZINAZOMFANYA ATUMIE BANGI



NAYE MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA MHE OMAR KHAMIS OTHMAN AMESEMA SERIKALI INAKATAZA MATUMIZI YA BANGI NA KUSEMA KWAMBA MTU AKITILIWA MASHAKA NA VYOMBO VYA ULINZI NI LAZIMA APEKULIWE.

No comments