MAAFISA UTUMISHI WANAOCHEZEA KUMBU KUMBU ZA WAFANYAKAZI WANYOOSHEWA VIDOLE
Pemba
AFISA
Mdhamini Ofisi ya Rais Katiba , Sheria , Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Pemba Massoud Ali Mohd amewaonyeshea
vidole maafisa Utumishi wanaochezea
kumbukumbu za wafanyakazi na kusababisha kupoteza taarifa muhimu za
wafanyakazi katika Taasisi zao .
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na Maofisa Utumishi wa
Umma katika Kikao cha Utekelezaji wa
Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma
huko Ukumbi wa Wizara ya Katiba na
Sheria Chake chake Pemba.
Amesema
kupotea kwa Kumbukumbu za Wafanya kazi
kunasababisha hasara kwa Serikali kwa kuendelea kuwa na
Rasili mali watu ambao hawanatena uwezo
wa kufanya kazi.
Aidha
Amesema Ofisa Utumishi ambaye atabainika kuzichezea kumbukumbu za
wafanyakazi na kusababisha mtumishi kuendelea kuwepo kazini kinyume na
sheria pamoja na kukatisha muda wa utumishi kwa
mtumishi atakumbana na mkono wa
sheria.
Nao
baadhi ya Watumishi waliohudhuria Mkutano
huo wamemtaka Afisa Mdhamini kutembelea
Mawizarani na kutoa elimu ya Utunzaji wa
Kumbukumbu.
Post a Comment