WAZIRI ABAINI UPOTEVU WA MAPATO YA SERIKALI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATENDAJI WA BARAZA LA MJI
Pemba.
WAZIRI wa Nchi
, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ, mhe
HAJI OMAR KHEIR amebaini upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali
yanayofanyika katika baraza la mji wete, kwa baadhi ya watendaji kutumia
risiti za iliyokuwa halmashauri ya wilaya hio na kujipatia fedha kwa maslahi
yao.
Amesema
Serikali inataarifa kamili ya ubadhirifu huo unaofanywa na baadhi ya
watendaji wa baraza hilo na kuikosesha Serikali mapato ambayo yalikuwa yatumike
katika kuleta maendeleo ya wananchi.
Mh.Waziri
ameyasema hayo, katika mkutano wa kukumbushana majukumu na watendaji wa
Serikali wakiwemo Madiwani , halmashauri na Wilaya ya Michheweni , Baraza la
Mji Wete, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Wakuu wa Wilaya pamoja
na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jamhuri .
Amesema
,Serikali haitamfumbia macho na kumuhurumia mtendaji yoyote anaejihusisha na
udanganyifu wakati wa kuwapatia huduma wananchi kwa njia zisizo halali kwa
maslahi binafsi.
Sambamba nahayo
amesema Wizara yake iko tayari kuwatoa kazini wanaothubutu kufanya vitendo
hivyo kwa nia ya kuondoa kasoro zilizopo na kuweka sawa utekelezaji wa majukumu
yao kwa maslahi ya nchi wanayoitumikia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, amewataka watendaji wa Halmashauri na
mabaraza kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kujua majukumu yao katika kufikia
dhamira ya kuingizia mapato Serikali
Post a Comment