Alietorosha Msichana Asakwa, Mnajisi Ahojiwa Polisi
NA
HAJI NASSOR, PEMBA
JESHI
la Polisi mkoa wa kusini Pemba, linamtafuta kijana Mohamed Nassor (25) mkaazi
wa Changaweni wilaya ya Mkoani, akituhumiwa kumtorosha msichana (16), aliechini
ya uangalizi wa wazazi wake.
Kamanda wa Polisi
Mkoani humo, Shehan Mohamed Shehan, alisema kijana huyo, alitoroka baada ya
kushitukia kuwa anafautwa na Polisi, baada ya kufanya kosa hilo.
Alisema kijana huyo
alikwenda kijiji cha Makombeni Oktoba 23, na alipofika, alimtorosha msichana
huyo na kumpeleka Changaweni kwa lengo la kumingilia.
Alisema baada ya mtoto
huyo kuhojiwa, ndipo taarifa zilipowafikia na kuanza kumtafuta, ingawa taarifa
za awali zilionyesha amekimbia.
“Jeshi ka Polisi
linamtafuta kila kona, na limeshaweka mitego, ili kuhakikisha anapatikana na
kufika mbele ya mkono wa sheria kujieleza”,alisema.
Hata hivyo amewataka
wazazi na walezi, kuwa karibu na watoto wao, na kila baada ya muda kujua
walipo, ili kuweza kutatua changamoto kama hizo zinapowatokea.
Wakati huo huo Jeshi
hilo la Polisi Mkoani humo, linaendelea kumuhoji kijana Juma Abdalla Salum
(29), mkaazi wa mjini Chakechake, kwa tuhuma za kumuingilia Ng’ombe jike.
Alisema kijana huyo
alietenda kosa hilo Oktoba 23, majira ya saa 12:30 jioni eneo la Ngoma hazingwa
nje kidogo ya mjini wa Chakechake,ambapo alionekana na watu na kisha kufikishwa Polisi.
Kamanda Shehan alisema,
baada ya kufikishwa Jeshi la Polisi linaendele kumuhoji na ikiwa ataonekana
anahusika na tukio hilo, jalada lake litafikishwa kwa DPP kwa ajili ya
uchunguzi na kisha kupanda mahakamani.
“Tukimaliza taratibu za
kumuhoji, linalofuata ni kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma
zinazomkabili za kumuharibu mnyama”,alifafanua.
Hili ni tukio la pili
kwa mwaka huu wa 2017, la kumuingilia mnyama, ambapo tukio la kwanza lililtokea
miezi minne iliopita, shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake.
Post a Comment