DPP asifia ushirikiano ZLSC
OFISI
ya Mkurugenzi wa Mashitaka kisiwani Pemba, imesifia sana ushirikiano uliopo,
baina yao na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, katika
kuwafikia wananchi kuwapatia elimu ya sheria, inayowapa ujasiri wa kudai haki
zao.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwanasheria wa Serikali kutoka Afisi hiyo, Juma Ali Juma wakati akizungumza
kwenye kipindi maalumu kilichorushwa na kituo kimoja ya redio, kisiwani Pemba
wakiwa na Afis Mipango wa Kituo cha hicho, Khalfan Amour Mohamed.
Alisema ZLSC,
mewasaidia sana wao kama ofisi ya DPP, kwa vile wamekuwa wakishirikiana kutoa
elimu hata ule wakati, ambao ofisi yao haijapata uwezo wa kwenda vijijini.
Mwanasheria huyo,
alisema inatokezea Kituo cha huduma za sheria, kuwa na safari za vijijini,
hivyo watendaji wa DPP huangana nao, hivyo kuwaelezea wananchi kazi na majukumu
yao.
Alisema, kuwepo kwa
ZLSC inaonyesha sasa wananchi baadhi wameshawiva kitaaluma walau kujua haki
zao, kutokana na wengine kupata ujasiri wa kufuatilia haki zao ofisini kwao,
jambo ambalo, awali lilikuwa gumu.
“Mimi nadhani
usirikiano wetu uliopo baina yetu sisi na ZLSC, umezaa matunda sana, maana
tunaona wananchi wanapofika hata mahakamani, wanajitetea kisheria sio maneno
matupu”,alifafanua.
Hata hivyo Mwanasheria
huyo wa serikali, amewataka wananchi kuendelea kuitumia ofisi yao, ili kupata
ufumbuzi wa mambo yao ya kisheria, badala ya kusikiliza maneno ya vijiweni.
Nae Afisa Mipango wa
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed,
alisema kituo kimekuwa na kazi kubwa ya kuwafikisha taaluma ya sheria wananchi.
Alisema, sasa wananchi
kadhaa wamepata uwelewa mkubwa wa kuzifuatilia haki zao kwenye vyombo vya
sheria, wakiwa na uthubutu jambo, ambalo hapo awali halikuwepo.
“Sasa wananchi
wanauwelewa mkubwa wa kuzitambua haki zao, tofauti na zamani na sasa wakienda
mahakamani, DPP au kwenye taasisi nyengine za kisheria, hili tunajivunia”,alisema.
Baadhi ya wananchi
walizoungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema taasisi za kisheria lazima
ziongeze kasi ya kuwaelimisha wananchi juu ya namna bora kujenga uthubutu ya
vyombo vya sheria.
Ali Hamza Haji wa
Machomane Chakechake, alisema pamoja na wananchi kupata, uwelewa lakini bado, vyombo
hivyo vinakumbwa na harufu ya rushwa.
Kwa upande wake Hassina
Hamad Omar, alisema wanawake lazima wajengewe uwezo wa kuvifikia vyombo vya
sheria, wanapokuwa wamedhulumiwa haki zao.
Hata hivyo wananchi
hao, waliwataka wanasheria kuhakikisha wanavitumia vyombo vya habari kutoa
elimu, ili wananchi wazidi kufahamu haki na wajibu wao.
Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka Zanzibar imeanzishwa mwaka 2002, sawa na Kituo cha Huduma za Sheria
kilichoanzishwa mwaka 1992 na kuanza kazi zake rasmi kisiwani Pemba, mwaka
2002.
Post a Comment