Header Ads

Madudu yabainika Ukaguzi wa WAKALA wa Chakula , Dawa na Vipodozi Zanzibar Ofisi ya Pemba

Image result for WAKALA wa Chakula , Dawa na Vipodozi Zanzibar Ofisi ya Pemba
WAKALA wa Chakula , Dawa na Vipodozi Zanzibar Ofisi ya Pemba imefanya ukaguzi kwenye maduka yanayouza vyakula pamoja na dawa za binadamu na kubaini kuwepo na mapungufu  ya badhi ya vyakula katika maduka hayo .
Akizungumza ofisini kwake Wete ,Mkaguzi wa Wakala Mohammed Said Abdalla amesema mapungufu ambayo yalibainika wakati wa ziara hiyo ni vyakula  vingi vya vinywaji kumalizika muda wa matumizi yake , huku wafanyabiashara kuendelea kuviuza.

Amesema kuwa katika ziara hiyo  wakaazi wa Wilaya ya Micheweni ndiyo wamebainika kutumia vyakula ambavyo vimepitwa muda wa matumizi yake hususani vyakula vya vinywaji .

Amesema kuwa Wakala ilichukua hatua ya kuviangamiza vinywaji hivyo ambavyo vilibainika kmalizika kwa  muda wa matumizi yake .

Aidha Mohammed pia amewataka wananchi pamoja na wafanyabiashara kuwa na kawaida ya kuzikagua bidhaa zao ili wakibaini vipo ambavyo muda wa matumizi umamalizika wachukue hatua ya kuviangamiza .

Ameeleza kwamba utamaduni huo utasaidia kudhibiti bidhaa ambazo zimemakliza muda wa matumizi kuendelea kukaa sokoni na hivyo kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi ya vyakula ambavyo vinaweza kusababisha athari katika maisha yao.

Naye Suleiman Faki Hamad mkaguzi kutoka Wakala wa Chakula , Dawa na Vipodozi Pemba amewataka wafanyabiashara kusajili biashara zao katika Ofisi ya wakala   na kuacha kufanya biashara bila ya kusajiliwa .

Amesema ni jambo jema kwa mfanyabiashara kuendesha shughuli zake bila ya kusajiliwa kwani kunaikosesha mapato Serikali ambayo yangerejea kwa jamii na kusaidia shughuli nyengine za maendeleo.

Amesema Wakala iko kisheria ambapo inajukumu na wajibu kisheria kumchukulia hatua za kisheria mfanyabiashara ambaye atabainika kukiuka misingi ya kisheria ikiwemo ni pamoja na kuendesha biashara bila ya kusajiliwa.

No comments