Header Ads

Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo awapa Siri Wafanyakazi Kituo cha Redio Micheweni Pemba



Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utali,Utamaduni na Michezo Juma Mjaja amewataka wandishi wa kituo cha Redio Jamii Micheweni kuzifuatilia na kuzipa kipaumbele taarifa kutoka ndani ya wilaya hiyo.

Rai hiyo ameitoa leo katika ofisi za redio jamii Micheweni wakati wa mahojiano maalum juu ya mfumo wa utayarishaji wa taarifa katika kituo hiki.
Amesema kuwa taarifa za wilaya ya Micheweni zinatakiwa kupewa kipaumbele zaidi katika kituo hiki kwani zinawasaidia wananchi kufahamu kile kinachoendelea katika jamii.

Aidha katika hatua nyingine Mjaja, amewataka wandishi hao kuendelea kuzingatia maadili ya uandishi ikiwemo matumizi sahihi ya lugha katika uandishi wa habari zao.

No comments