RC Kas Pemba Ahimiza Wakulima wa Mpunga Mkoani Humo Kuzitumia Trekta
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewataka wakulima wa mpunga wa mabonde ya
Chanjaani Konde na Koowe kuchangia gharama za kulimiwa ili matrekta yafanye
kazi kwa mpangilio .
Akizungumza na baadhi ya
wakulima pamoja na maafisa kutoka Idara ya Kilimo Pemba amesema matrekta
yanapaswa kulima bonde moja kwa pamoja ili yaendelee katika mabonde mengine.
Mhe Omar ameyasema
hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua kilimo cha kunde pamoja na maandalizi
ya kilimo cha mpunga ambapo amewataka kushirikiana na watendaji wa wizara ya
kilimo ili kufanikisha lengo .
Naye kaimu Mkuu wa Idara ya
Kilimi Pemba Juma Maalim Faki amesema jumla ya ekari 8059.75 sawa na asilimia
79.01 ya lengo la ekari 10200 la Mkoa zimechimbuliwa kwa jembe la mkono na
trekta.
Naye mwenye wa Bonde la
Koowe Faki Khamis Faki amesema wakulima wa bonde hilo wameweza kunufaika na
elimu inayotolewa na mabwana / mabibi shamba ambao wamekuwa karibu na wakulima
wa bonde hilo.
Post a Comment