Header Ads

Ukaguzi wa Vyoo Waibua Kaya 36 kutokuwa na Vyoo Bora Iringa

Image result for Vyoo Bora Image result for Vyoo Bora

ZAIDI ya kaya 36 kijiji cha Isakalilo Wilaya ya Iringa zimewekwa bendera nyekundu zinazoashiria kutokuwa na choo bora.

Kukosekana kwa vyoo katika nyumba hizo kunaweza kusababisha wakazi wake kupata maradhi ya mripuko ikiwemo matumbo ya kuharisha na kipindupindu.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamemwambia mwandishi wa habari hizi kwamba wanashindwa kuchimba vyoo na kuvitumia kutokana na kukabiliwa na hali ya umaskini.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa vyoo bora Mtendaji wa kijiji cha Isakalilo bwana Majeshi Richard  Ndambo amesema kaya 4 hazikuwa na vyoo kabisa na zingine 36 waliweka bendera nyekundu kwa kutokuwa na choo bora.

Amesema katika ukaguzi nyumba ambazo zimebainika kutokuwa na vyoo tumelazimika kuzipachika bendera , ili kuonyesha kwamba Serikali ya kijiji imekusudia kuimarisha matumizi sahihi ya vyoo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina  Masenza amesema swala la vyoo bora linakwenda sambamba na lishe bora ambalo hupelekea utapia mlo kuwa juu mkoani hapa.

Ameshauri uongozi wa Serikali ya kijiji hicho kuanzisha mashindano ya utumiaji wa vyoo na kutoa motisha kwa kijiji ambacho kitafanya vizuri jambo ambalo litazidi kuwahasisha wananchi kuzingatia matumizi ya vyoo.

"Nakushauri uanzishe mashindano ya utumiaji wa vyoo katika kijiji ambapo kijiji ambacho kitafanya vyema kipewe motisha "alishauri
.
Halikadhalika wakati wa ukaguzi huo Masenza amebaini hali ya uchafu katika kijiji hicho ikiwa zimepita siku chache tu za siku ya usafi.
Na Massanja Mabula

No comments