UNESCO: Tumieni Kituo cha Redio Micheweni Kutatua Changamoto Zenu
mwezeshaji wa mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na UNESCO, Rose Haji Mwalim akitoa mafunzo kwa washiriki wa mafunzo hayo. |
Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeitaka jamii ya watu wa Micheweni
kukikumia kituo cha redio jamii micheweni ili kufikisha taarifa za mambo
mbalimbali yanayojitokeza katika jamii kila siku.
Rai hiyo imetolewa na
mwezeshaji wa mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike
yanayoendeshwa na UNESCO, Rose Haji Mwalim, yanayoendelea katika Ukumbi wa
Skuli ya sekondari Chwaka Tumbe
Akiwasilisha mada ya
elimu ya utayarishaji wa vipindi vya redio kwa washiriki, Mwalim Rose amesema
kuwa walimu wakishirikiana na wanafunzi pamoja na wazazi kupitia vyombo vya
habari wanaweza kutatu changamoto zinazowakabili ikiwemo, unyanyasaji wa
kijinsia, ubakaji na ulawiti.
Akizitaja baadhi ya
mambo ambayo yakuwa yakirudisha maendeleo ya micheweni amesema kuwa ni,
kutokuwepo kwa elimu tosherezi ya afya ya uzazi, ubakaji pamoja na ulawiti.
Kwa upande wake mwalimu
mshiriki wa mafunzo hayo, Hamad Mbwana Shaame, amelipongeza shirika la UNESCO
kwa kutoa elimu hiyo kwa vijana wa Micheweni kwani itawasaidia kupambana na
changamoto ambazo zimekuwa zikiikabili jamii ya micheweni kwa siku za hivi
karibuni.
Mafunzo
ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na
UNESCO yana lengo la kuunda Vikundi vya Vijana Shuleni na Akina Mama
Watayarishaji Vipindi vya redio kwa kushirikiana na Redio Jamii Micheweni,
ambavyo vitasambaza Elimu rika kwa Vijana na Akina Mama.
Post a Comment