WANAFUNZI Washiriki Mafunzo ya UNESCO Wapewa Siraha Kujikinga na Mimba za Utotoni Micheweni
Wanafunzi kisiwani
Pemba wametakiwa kutojihusisha katika mapenzi ya umri mdogo ili kuepukana na
matatizo mbalimbali ikiwemo mimba za umri mdogo.
Rai hiyo imetolewa na
mwezeshaji wa mafunzo ya kuwawezesha wanafunzi uelewa juu ya masuala ya afya ya
jamii na ushiriki katika uandaaji wa vipindi vya Redio, Suleiman Fakhi Haji, yanayoendelea katika
Ukumbi wa Sikuli ya sekondari Chwaka Tumbe.
Mwezeshaji huyo amesema
kuwa katika kipindi hiki wanafunzi wanatakiwa kuzingatia masomo yao ili waweze
kufanikiwa kutimiza ndoto zao.
Aidha ameongeza kuwa
katika siku za hivi karibuni kutokana na kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii
wazazi wamekuwa ndio kisababishi cha kupelekea watoto kufanyiwa vitendo vya
udhalilishaji ikiwemo ulawito.
Kwa upande wa mzazi
anaeshiriki mafunzo hayo, Bi Time Juma amewataka wazazi wenzake kuwa msitari wa
mbele katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji ikiwemo mapenzo ya umri
mdogo kwa watoto wao.
Mafunzo ya kuwawezesha
wanafunzi uelewa juu ya masuala ya afya ya jamii na ushiriki katika uandaaji wa
vipindi vya Redio yanayo endelea katika Ukumbi wa Sikuli ya sekondari Chwaka
Tumbe yanajumuisha wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Micheweni, Tumbe, Wingwi
na Chwaka Tumbe, Walimu pamoja na Wazazi.
Post a Comment