MABODI: Mafanikio ya SMZ ni kiashiria tosha cha juhudi za Kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar
NAIBU Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkk.Abdalla Juma Saadalla'Mabodi'. |
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema mafanikio yliyofikiwa na Serikali ya
awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ni kielelezo tosha cha kuenzi kwa vitendo Mapinduzi hayo ya Januari 12, mwaka 1964.
Udhibitisho huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ wakati akitoa tathimini yake juu ya
hotuba ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein aliyoitoa katika kilele cha wamaadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya
Mapinduzi zilizofanyika Uwanja wa Amaan
Mjini hapa.
Dk. Mabodi alisema mambo yaliyotajwa katika hotuba
hiyo ni sehemu ya mafanikio ambayo kila mwananchi anatakiwa kujivunia kwani ni
hatua ya maendeleo yanayotokana na utekelezaji
mzuri wa Ilani ya Uchaguzi CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote.
Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza mambo mbali mbali ya
kimaendeleo bila kujali changamoto na vikwazo vya kisiasa kwa lengo la
kurahisisha upatanaji wa huduma za msingi kwa wananchi waliopo mijini na
vijijini.
Alieleza kuwa mambo yaliyotolewa ufafanuzi wa kina
ndani ya hotuba hiyo ya Dk.Shein ni pamoja na kuimarika kwa sekta ya uchumi
ambapo makusanyo ya mapato yamefikia shilingi bilioni 548.571 kwa mwaka 2017
ikilinganishwa na shilingi bilioni 487.474 zilizokusanywa katika mwaka 2016.
Alisema kwa mujibu wa hotuba hiyo imetaja kasi ya
ukuaji wa uchumi kwa bei halisi imekua kwa asilimia 7.0 kwa mwaka 2017,
ikilinganishwa na asilimia 6.8 kwa mwaka 2016, hatua inayopongezwa na Chama cha
Mapinduzi Zanzibar.
Naibu Katibu mkuu huo anaendelea kueleza kuwa kutokana
na juhudi za serikali chini ya usimamizi wa CCM pato la mtu mmoja limetajwa
kufikia shilingi 1,806,000 ikilinganishwa na shilingi 1,632,000 kwa mwaka 2015.
Pia alieleza kuwa kasi ya mfumuko wa bei imefikia asilimia
5.6 katika mwaka 2017 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2016.
“Mafanikio yote hayo ni miongoni mwa utekelezaji wa
ahadi tulizotoa kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu wa dola uliopita kwa
hiyo tunaendelea kutekeleza kwa kasi
kubwa ili ikifikia uchaguzi mkuu ujao tuwe tupo katika kiwango cha kuridhisha
katika utatuzi wa kero za wananchi.”, alisema Dk.Mabodi.
Alisema lengo
la serikali ni kuhakikisha ni kuimarisha uchumi,kupunguza umasikini na kuifanya
Zanzibar kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kiwango cha kati ifikapo mwaka
2020 huku ikijipanga kufikia kiwango cha nchi za visiwa zilizoendelea duniani.
Dk.Mabodi aliisifia serikali kwa hatua zake za miradi
mikubwa 25 ambayo ikikamilika itatoa ajira 915 kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar.
Akizungumzia sekta mama ya Utalii nchini alisema
katika hotuba ya Dk.Shein imeweka wazi kuimarika kwa Nyanja hiyo ambayo
imeingiza jumla ya watalii 433,116 nchini katika kipindi cha mwaka
2017,ikilinganishwa na idadi ya watalii 379,242 walioingia nchini katika mwaka
2016 ambalo ni ongezeko la asilimia 14.2.
“Sina shaka na ahadi ya Rais wetu mpendwa Dk.Shein ya
Serikali kufikia idadi ya watalii 500,000 ifikapo mwaka 2020”,, Dk.Mabodi alipongeza
juhudi hizo na kutoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha
dhana ya utalii kwa wote.
Pamoja na hayo Dk.Mabodi alisema serikali chini ya
usimamizi wa CCM imekuwa mstari wa mbele
kuimarisha sekta ya Elimu ambayo ni chimbuko na uti wa mgongo wa maendeleo ya
nchi yoyote duniani kwa kuzalisha wataalam wa fani mbali mbali wanaosaidia
kutekeleza sera za kisiasa ili ziendane na mahitaji halisi ya wananchi.
Kupitia tathimini ya hotuba hiyo Dk.Mabodi alisifia
tamko la Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed
Shein la kuwatangazia wananchi kuwa kuanzia mwezi wa Julai 2018, serikali
itaanza kutekeleza azma ya kurudisha utaratibu wa elimu bure kwa ngazi za
msingi na sekondari ili kutekeleza
shabaha ya Mapinduzi.
Mbali na tamko hilo pia Dk.Mabodi alisema CCM inaunga
mkono msimamo wa Serikali kutoa pencheni jamii kwa wazee wote waliofikia umri
wa miaka 70 , bila kuzingatia kazi walizokuwa wakifanya ambapo jumla ya wazee 27,627 wamelipwa jumla
ya shilingi bilioni 10.175 tangu utaratibu huo umeasisiwa mwezi April 2016, kwa kila Mzee kupewa sh.20,000 kwa mwezi.
Post a Comment