RC kusini Pemba: Nitakula sahani moja na masheha wanajivisha koti la uhakimu kesi za udhalilishaji
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe: Hemed Suleiman Abdulla, mewajia juu masheha wa mkoa wake kwamba, watakosa kazi mara moja na kisha sheria kufuata mkondo wake, iwapo hawatoiwacha tabia yao ya kujifanya mahakimu kwa kuzifanyia sulhu kesi za udhalilishaji.
Alisema
kuanzia sasa katika kutokomeza matedo hayo ndani ya mkoa wake, masheha wanaovaa
koti la uhakimu, walivue mara moja, maana hilo haliisaidia jamii kupunguza
matendo hayo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari ofisini kwake katika kutomeza matendo hayo, alisema kama
wapo masheha wanafanya sulhu, basi sasa wakati umefika wa kubadili tabia hiyo,
vyenginevyo hatua dhidi yao itafuata.
Alisema, kwa
sasa Mkoa umeshaunda kamati maalumu ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia, hivyo
kila mmoja wakiwemo hao masheha lazima wakijite katika kumaliza kesi hizo kwa
kuzisimamia hadi vyombo vya sheria.
“Masheha wao
kazi yao kwenye kesi hizi za udhalilishaji zenye sura ya jianai,
wazishughulikie na kuzifikisha mbele ya vyombo vya sheria, ili wakosaji wapate
hukumu”,alisema.
Katika hatua
nyengine Mkuu huyo wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe: Hemed Suleiman Abdulla, alisema
lazima kila mmoja kwa nafasi yake, iwe ni Jeshi la Polisi, waendesha mashitaka,
jamii na mahakimu, wawajibike ili kutokomeza matendo hayo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa huo, Shehan Mohamed Shehan alisema, jamii inayonafasi kubwa ya kutokomeza matendo hayo, kwa kukubali kufika
mahakamani, kutoa ushahidi.
Alisema
vyombo vya sheria pekee haviwezi kutokomeza vitendo hivyo, pasi na jamii
kushirikiana na mahakama kutoa ushahidi kwa wakosaji.
“Leo
wananchi huwa wakali wakianza kupata kesi ya udhalilishaji, lakini ikifika siku
ya kutoa ushahidi mahakamani, huanza kujitia sababu na hatimae kesi kufutwa kwa
kukosa ushahidi”,alieleza.
Kwa upande
wake Mwansheria dhamana wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Ali Rajab Ali,
alisema jamii ndio pekee ambayo ina nafasi kubwa ya kutokomeza matendo hayo.
“Kama
wakijipangia mikakati ya kweli na kushirikiana kikamilifu na vyombo vya sheria,
basi itakuwa ni dawa mwafaka ya vitendo vya udhalilishaji kama ubakaji au
ulawiti kumaliza”,alifafanua.
Mratibu wa
wanawake na watoto shehia ya Kangagani Awena Salim Kombo, alisema tatizo la
jamii kutopenda kutoa ushahidi kwa changamoto zilizoko mahakamani, hakusaidia
kutokomeza vitendo hivyo.
Mzazi ambae
mwanawe alifanyiwa ulawiti wa shehia ya Kiungoni alisema, changamoto kubwa
inayodhoofisha kuzimaliza udhalilishaji, ni Jeshi la Polisi kwa kuzifanyia
sulhu kesi hizo.
“Polisi
lazima wajipange vyema ili kuhakikisha, hawazifanyii sulhu kesi hizo, maana
kumekuwa na tuhuma za kuchukua rushwa na kuzimalizia kienyeji pale pake kituo
cha Polisi”,alifafanua.
Mratibu wa
miradi ya kutoka TAMWA Asha Abdi Makame, alisema sasa wakati kwa wakosaji wa
udhalilishaji, kupewa udhabu kali hadi kifungo cha maisha, ili kutomeza matendo
hayo.
“Wakosaji wa
matendo ya udhalilishaji, wamekuwa wakijirejea siku hadi hadi, kutokana na
adhabu wanayopewa mahakamani kuwa ndogo”,alisema.
Baadhi ya
watoto ambao walishafanyiwa udhalilishaji, wamependekeza kwa vyombo husika,
kuhakikisha wanawaadabisha wazazi na walezi wao, wanaozifanyia sulhu kesi hizo.
Afisa Ustawi
wa jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed, alisema udhalilishaji, hauwezi
kuondoka iwapo vyombo mbali mbali havikushirikiana kwa pamoja.
Sheha wa
shehia ya Shamiani wilaya ya Mkoani Safis Khamis Ngwali, alisema bado tatizo
lipo kituo cha Polisi, kwa kuwabembeleza waliodhalilishiwa, kufanya sulhu na
pande nyengine.
“Inawezekana
hawa Polisi wetu hawapendi kwenda mahakamani kutoa ushahidi na ndio maana,
hupendelea sana kesi za udhalilishaji zimalizike kienyeji pale pale
mapokezi”,alisema.
Hata hivyo
Katibu wa baraza la vijana shehia ya Chambani Zuwena Nassor Salum, alisema
vijana wasipotaka kubadili tabia na kuachana na matendo ya udhalilishaji
pasitarajiwe miujuzi ya kuvilamaliza vitendo vya udhalilishaji.
Katika
wilaya ya Wete pekee, kuanzia mwaka 2015 hadi mwezi Oktoba mwaka huu
kuliripotiwa matukio 600 za udhalilishaji, wakati 63 yalihusua ulawiti pekee,
ambapo na juzi kulikamatwa watoto 12 wakilawitiana.
Post a Comment