Header Ads

Wadau: “wanaofungwa kwa udhalilishaji wasipewe msamaha”

Image result for kesi za ubakaji na ulawiti 
KUTOLEWA msamaha kwa washtakiwa wa kesi za ubakaji na ulawiti, kunawapa nguvu yakuendelea wafanyaji wa matendo ya udhalilishaji na kupelekea kuongezeka siku hadi siku, wadau wa kupinga udhalilishaji wamesema.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa nyakati tofauti kisiwani Pemba walisema, washtakiwa wa makosa ya ubakaji na ulawiti hawahitaji msamaha, kwani ni wanaofanya ni jinai kubwa mithili ya mauwaji.

Walieleza kuwa, zipo kesi ambazo washtakiwa wanaweza kupatiwa msamaha, mfano wizi wa mazao au za kisiasa na sio kama za ubakaji na ulawiti, kwani ni kuvipalilia vitendo hivyo viendelee katika jamii.

“Kwa kweli wanapopewa msamaha washtakiwa wa kesi za ubakaji na kulawiti, ni kuwashawishi wenye tabia za hizo kuendelea kuwadhalilisha watoto wetu, kwani wataona hayana nguvu yoyote makosa hayo”, walisema wanajamii hao.

Mmoja wa wananchi hao, Bimize Omar Massoud (30) mkaazi wa Kifumbikai Wete alieleza kuwa, iwapo kesi za ubakaji na ulawiti zitakuwa na msamaha kwa washitakiwa, vitendo vya udhalilishaji kwa watoto vitaendelea.

“Mtoto ndio taifa la kesho na ndio viongozi wapya, wanahitaji kuenziwa na suala la kubaka na kulawitiwa sio dogo, hivyo kesi hizi zitiliwe uzito na wasipewe msamaha wa rais wala wa mwanasheria mkuu, kwani vitendo vitaendelea”, alieleza mwananchi huyo.  

Nae Omar Abdalla Hamad (70) mkaazi wa Chasasa Wete alisema kuwa, washtakiwa wa matendo ya ubakaji na ulawiti hawastahiki kupewa msamaha, kwani kitendo hicho ni cha kinyama anachomfanyia moto asiewe na uwelewa.

“Mimi nadhani sio sahihi washtakiwa wa matendo ya ubakaji na ulawiti nao kuwemo kwenye orodha ya washitakiwa,  kupewa msamaha, kutokana na kuwa kitendo hicho ni cha kikatili na unyanyasaji wanaofanyiwa watoto wetu” ,alisema.

Kwa upande wake mwandishi wa habari wa redio jamii Mkoani Shaib Kifaya Omar, alisema kuwa, washitakiwa wa makosa hayo hawahitaji msamaha na badala yake watumikie chuo cha mafunzo mpaka imalize adhabu yao.

Mkaazi wa Jadida Wete, ambae hakutaka jina lake lichapishwe ambae mwaka jana mwanawe alilawitiwa, alieleza kuwa, sheria bado zinahitaji kurekebishwa, ili zisiweke kifungu cha kumpa kiongozi mamlaka ya kutoa msamaha kwenye makosa ya udhalilishaji.
“Iwepo misamaha lakini sio kwa kesi za udhalilishaji kama ulawiti, maana sasa wataendelea kuwakatili na kuwabaka watoto na kuwapotezea malengo yao ya baadae, jambo ambalo linatuumiza sana”, alisema mwananchi huyo.

Said Abrahman Salim (33) mkaazi wa Wete alisema kuwa, sio kutolewa misamaha kwa kesi hizo, kwani wafanyaji watajenga kuwa baada ya muda mfupi watatolewa, jambo ambalo litakwamisha juhudi za kutokomeza matendo hayo.

Mkubwa Hassan Haji (17) wa Mtambile, alisema kama washitakiwa hao walivyokosa huruma na kisha kuwabaka au kuwalawiti, basi sio vyema wao wakapewa msamaha.

Sheikh Nassor Said Abdalla wa mjini Chakechake, alisema asiependa kuwahurumia wengine nay eye sio vyemma kupewa fungu la huruma, kama ilivyo sasa kwa kupewa msahama.

Kwa upande Mratibu wa wanawake na watoto, shehia ya Kangagani, Awena Salim Kombo, alieleza kuwa ni jambo la kusikitisha kwa washtakiwa wa makosa ya ulawiti na ubakaji, kuingia katika ya washitakiwa wanaopaswa kupewa dhamana.

 Nae Mratibu wa shehia ya Kinyikani Mauwa Said Khamis alisema kuwa ni vyema kwa serikali kuliangalia suala hilo kwa upana zaidi na kuepuka kutoa msamaha kwa washitakiwa wa makosa hayo.

 Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Pemba, Khatib Juma Mjaja, alieleza kuwa, wakati umefika kwa kesi hizo, zisingiliwe na kiongozi yeyote kwa lengo la kutoa msahama. 

 “Wakitoka gerezani washitakiwa hawa, jamii nzima hushituka na kuona kwamba watoto wao wanakuja kumalizwa, kutokana na kuwa katika magereza hawapewi mafunzo ya kuachana na vitendo hivyo”, alieleza Afisa huyo.

Mratibu wa Kituo cha Mkono kwa Mkono Chakechake Arafa, alisema sio vyema kuwepo kwa msamaha na ikiwezekana wawe na kifungo cha maisha chuo cha mafunzo.

“Mamlaka ya rais ya msamaha yaendelee kuwepo, lakini kwa vile anashaurika, basi aambiwe kuwa hawa wanaokabiliwa na vitendo vya udhalilishaji asiwaguse”,alishauri. 

Mratibu wa miradi kutoka TAMWA Asha Abdi, anasema ili katika kutomeza matendo hayo, lazima muhimu wa mahakama usiingiliwe baada ya kutoa hukumu.

“Kama mshitakiwa anafungwa miaka 10, au saba basi ni vyema aachwe mpaka amalize, na huruma kwa watu hawa isiwepo, maana wameshaliumiza taifa”,alisema.

Wakili wa kujitegemea kisiwani Pemba Zahran Mohamed Yussuf, alisema suala la msamaha kwa washitakiwa walioko magarezani ni haki yao, kama zilivyo haki mwengine kwa makundi ya watu.

“Kwangu mimi sijaona tatizo sana kupewa msamaha, maana inawezekana ana magonjwa, hajimudu kikazi hivyo ni haki yake maana hiyo ni mamlaka ya kiongozi ndani ya nchi yake”,alisema.
Afisa Mdhamini anaeshughulikia wanawake na watoto Khadija Khamis Rajab, alisema wakati serikali ikiweka mikakati ya kumaliza udhalilishaji, lazima na hili la msamaha kwao lifutwe.

“Lazima kuwe na sheria maalum, inayowakataa hawa wanaofungwa kwa udhalilishaji, wasipewe msamaha na waendelee kuishi chuo cha mafunzo mpaka wamalize haki yao ya kifungo”,alishauri.

Uchunguuzi wa uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini kuwa washitakiwa 16 kisiwani Pemba walipata msamaha wakikabiliwa na makosa kadhaa kuanzia mwaka 2014 hadi mwezi Disemba mwaka jana.

Ambapo kwa mwaka 2014, walikuwa washitakiwa wanne (4), mwaka uliofuata ni saba (7) na kuanzia Januari hadi mwezi Disemba mwaka 2016 walikuwa washitakiwa watano (5).

1 comment:

  1. UDkt James ungudokotela wamakhambi owangiphilisa ngegciwane lengculazi, engathinta kulo nyakenye ngoFebhuwari, ngikhathazeke kakhulu ngegciwane elingaphakathi kimi, lapho ngiya esibhedlela ngiyohlolwa ukuthi ngine-HIV, ngaphuza izidakamizwa ezahlukahlukene nomjovo namanje Angikelapheki, ngaze ngathola othile owathola ubufakazi bokuthi welashwa kanjani i-HIV evela kudokotela James herbalxube, ngacabanga ukuthi ngamanga, kepha ngathola isasasa ngaxhumana noDkt James ku-imeyili yakhe, i-drjamesherbalmix @ gmail.com
    Futhi ngamtshela inkinga yami futhi wangibuza imibuzo ethile futhi ngaphendula ke wathi angingakhathazeki ukuthi uzongisiza, futhi welapha ne-HIV yami. Ngijabule kakhulu ezinsukwini ezingama-2 kamuva wangithumelela ikhambi ngokusebenzisa insizakalo ye-DHL, ngaqala ukusebenzisa umuthi ekuseni nakusihlwa njengoba angibhalela amasonto amathathu, lapho ngiyobheka ukuthi ngihlolelwa i-HIV njalo ngenyanga ujabule futhi ujabule kakhulu ngenxa yokukhululeka kwi-HIV.
    Ngihlanganyela lobu bufakazi ngoba ngiyazi ukuthi bekunzima kanjani kimi ukulala futhi ngicabanga nsuku zonke ngokuba ne-HIV ngacishe ngazibulala kepha Indoda enkulu le uDkt James yabuyisela impilo yami emuva. Ngiyazi ukuthi kusenabantu lapha abane-HIV noma yiluphi uhlobo lwezifo ezifana ne-DIABETES, Cancer, HANGALANI IMIPHUMELA, I-BOWEL OBSTRUCTION, HIV / AIDS, HERPES, HEPATITIS A&B, CARDIAC DisEASES, CHRONIC DisEASES, YELLOW FEever, EPRIPE, STROKE I-SPINAL CORD, ECZEMA, IZIFO ZESIFUNDA, I-ACME, IPHUPHA NGEMPELA, I-DENGUE SCHIZOPHRENIA, i-APOLLO, I-SCLEROSIS E-BLOOD PRESSURE, UKUVUNYELWA KWEMVELO, I-ArthRITIS, IMENINGITIS.
    drjamesherbalmix@gmail.com
    whatsApp +2348152855846  

    ReplyDelete